29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

DK. MAGUFULI KUFUNGUA KONGAMANO LA MAADILI

RAIS Dk. John Magufuli

Na CHRISTINA GAULUHANGA – DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli anatarajiwa kufungua kongamano la maadili  lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata).

Akizungumza kwa niaba ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Aboubakar Zuberi Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata, Sheikh Khamis Mataka, alisema kongamano hilo litafanyika Aprili 24.

Alisema lengo la kongamano hilo ni kujadili mmomonyoko wa maadili uliopo ndani ya jamii hivi sasa.

“Kongamano hili limeandaliwa na Bakwata ambapo litahudhuriwa na masheikh mbalimbali pamoja na viongozi wa kidini kutoka mikoa mbalimbali, lengo likiwa ni kuangalia jinsi maadili yalivyoporomoka na kutafuta mbinu ya kuijenga jamii iliyo bora,” alisema Sheikh Mataka.

Alisema kongamano hilo la siku moja litafungwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

Alisema wengine watakaohudhuria kongamano hilo ni wajumbe wa Ulamaa Taifa, masheikh kutoka taasisi mbalimbali, viongozi wa kidini kanda, mabalozi, wakuu wa vyombo vya usalama na wananchi walioalikwa.

Sheikh Mataka alisisitiza kuwa maadili ni muhimu ndani ya jamii na kwamba kwa sasa nchi inakabiliwa na mmomonyoko wa maadili.

“Ukiona jamii inazungukwa na walevi, watumiaji dawa za kulevya, binadamu wengine wanafurahia wenzao wakiuawa au kupata ajali, ni hali ya kupoteza mwelekeo wa maadili,” alisema Sheikh Mataka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles