NA WAANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza matokeo ya awali ya urais kwa majimbo 26, yakionyesha mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli anaongoza akifuatiwa na Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.
Matokeo hayo yalitangazwa jijini Dar es Salaam jana kwa nyakati tofauti na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva kutoka kituo kikuu cha kutangazia matokeo kilichopo katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere.
MAKUNDUCHI
Akitangaza matokeo ya Jimbo la Makunduchi lililoko Zanzibar, Jaji Lubuva alisema Dk. Magufuli alipata kura 8,406 sawa na asilimia 81.20 akifuatiwa na mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, aliyepata kura 1,769 sawa na asilimia 17.9.
Katika jimbo hilo, alisema waliojiandikisha walikuwa ni 12,742 na waliojitokeza kupiga kura walikuwa 10,682 sawa na asilimia 81.24.
Aliwataja wagombea wengine waliofuatia na kura zao kwenye mabano kuwa ni Hashim Rungwe – Chaumma (68), Lutalosa Yemba – ADC (58), Kasambala Marick -NRA (23) Anna Mghwira – ACT-Wazalendo (22), Macmilan Lyimo -TLP (18) na Fahmi Dovutwa – UPDP (18).
PAJE
Kwa upande wa Jimbo la Paje, Jaji Lubuva alisema Dk. Magufuli alipata kura 6,035 sawa na asilimia 81.20, Lowasa kura 1,899 sawa na asilimia 23.60 na kufuatiwa na ACT kwa kura 36.
Chaumma walipata 28, ADC kura 21, TLP na NRA kila moja kura nane na UPDP kura 7.
LULINDI
Katika Jimbo la Lulindi, Dk. Magufuli alipata kura 31,603 sawa na asilimia 71.28 na Lowassa kura 11,543 sawa na asilimia 26.03 ya kura zote halali.
Wengine ni Mghwira aliyepata kura 528, Lutalosa Yemba kura 362, Rungwe kura 179, Kasambala kura 43, Lyimo kura 45 na Dovutwa kura 34.
CHAMBANI
Jimbo la Chambani, Lowassa ameongoza kwa kupata kura 5,319 sawa na asimilia 83.90 akifuatiwa na Dk. Magufuli aliyepata kura 818 sawa na asilimia 12.90.
Rungwe alipata kura 63, Chief Yemba kura 50, Dovutwa kura 36, Kasambala kura 20, Lyimo kura 19 na Mghwira kura 15.
KIWANI
Lowassa ameongoza kwa kupata kura 4,229 sawa na asilimia 68.51 akifuatiwa na Dk. Magufuli kura 1,661 sawa na asilimia 12.9.
Mgombea wa Chaumma alipata kura 96, ADC kura 71 UPDP kura 39, NRA kura 28, ACT kura 27 na TLP kura 22.
NSIMBO
Dk. Magufuli ameongoza kwa kupata kura 31,413, Lowassa kura 6,042, mgombea wa ACT kura 183, ADC kura 64, Chaumma kura 42, UPDP kura 15, TLP kura 14 na NRA kura 6.
NDANDA
Katika jimbo hilo, Dl. Magufuli alipata kura 33,699, Lowassa kura 19,017, mgombea wa ACT- Wazalendo kura 594, ADC kura 409, Chaumma kura 189, UPDP kura 49 na TLP kura 49.
DONGE
Dk. Magufuli alipata kura 5,592, Lowassa kura 1,019, mgombea wa Chaumma kura 23, ADC kura 22, NRA kura 10, UPDP kura 7, ACT kura 5 na TLP kura 4.
KIWENGWA
Mgombea wa CCM, Dk. Magufuli alipata kura 3,317, Lowassa kura 1,104, Chaumma kura 27, ADC kura 24, TLP kura 19, ACT kura 15, UPDP kura 10 na NRA kura 9.
BUMBULI
Dk. Magufuli alipata kura 35,310, Lowassa kura 7,928, mgombea wa ACT kura 447, ADC kura 188, UPDP kura 25, NRA kura 15 na TLP kura 13.
KIBAHA MJINI
Mgombea wa CCM, Dk. Magufuli alipata kura 34,604, Lowassa kura 25,448, ACT kura 314, Chaumma kura 77, ADC kura 59, TLP kura 17, NRA kura 15 na UPDP kura 11.
MKOANI
Lowassa ameongoza kwa kupata kura 7,368, akifuatiwa na Dk. Magufuli kura 3,341, Chaumma kura 87, ADC kura 60, NRA kura 44, TLP kura 33, UPDP kura 27 na ACT kura 20.
MTAMBILE
Latika jimbo hili, mgombea wa Chadema, Lowassa amepata kura 5,875, Dk. Magufuli kura 902, Chaumma kura 56, ADC kura 41, UPDP kura 25, NRA kura 22, TLP kura 18 na ACT kura 7.
GANDO
Mgombea wa Chadema alipata kura 5,903, CCM kura 881, ACT kura 11, ADC kura 23, Chaumma kura 49, NRA kura 14, TLP 11 na UPDP 25.
MTAMBILE
Mgombea wa Chadema alipata kura 6,903, CCM kura 428, ACT kura 9, ADC kura 28, Chaumma kura 58, NRA kura12 , TLP 21 na UPDP 37.
MGOGONI
Mgombea wa CCM alipata kura 710, Chadema kura 6,506, ACT kura 12 , ADC kura 31, Chaumma kura 45, NRA kura 12, TLP 8 na UPDP 37.
KISARAWE
Mgombea wa CCM alipata kura 24,886, Chadema kura 13,093, ACT kura235 , ADC kura 19 , Chaumma kura 314, NRA kura 26, TLP kura 22 na UPDP kura 46.
MBINGA MJINI
Mgombea wa CCM alipata kura 29,225, Chadema kura 11,665, ACT kura 329, ADC kura 131 , Chaumma kura 66, NRA kura 10, TLP 16 na UPDP 16.
NANYAMBA
Mgombea wa CCM alipata kura 24904, Chadema kura 16992, ACT kura 361 , ADC kura 202 , Chaumma kura 172, NRA kura 39, TLP 48 na UPDP 64.
MOSHI MJINI
Mgombea wa CCM alipata kura 28,909, Chadema kura 49,379, ACT kura 149, ADC 186 , Chaumma kura 1,154, NRA kura 8, TLP 7 na UPDP kura 6.
MKINGA
Mgombea wa CCM alipata kura 23,798, Chadema kura 11,291, ACT kura 228, ADC kura 186, Chaumma kura 351 , NRA kura 31, TLP 29 na UPDP 27.
PERAMIHO
Mgombea wa CCM kura 32,505, Chadema kura11,291, ACT kura 359, ADC kura 135, Chaumma kura 66, NRA kura 16, TLP 15 na UPDP 22.
NJOMBE MJINI
Mgombea wa CCM alipata kura 33,626, Chadema kura 20,368, ACT kura 362, ADC kura111 , Chaumma kura 78, NRA kura 14, TLP 21 na UPDP 17.
SINGIDA MJINI
Mgombea wa CCM alipata kura 36,035, Chadema kura 19,007, ACT kura 235, ADC kura 87, Chaumma kura 64 , NRA kura 10, TLP kura 12 na UPDP kura 7.
LINDI MJINI
Mgombea wa CCM alipata kura 21,088, Chadema kura 17,607, ACT kura 123, ADC kura 103 , Chaumma kura 67, NRA kura 11, TLP 6 na UPDP kura 13.
WETE
Mgombea wa CCM alipata kura 958, Chadema kura 5,119, ACT kura 18, ADC kura 22 , Chaumma kura 28, NRA kura 15, TLP 16 na UPDP kura 10.