26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Kimei: Hali ya uchumi tete

Dk. Charles Kimei
Dk. Charles Kimei

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

BENKI ya CRDB imesema imepunguza kasi ya utoaji mikopo   kuangalia hali ya uchumi nchini inavyokwenda.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk. Charles Kimei, alisema kwa sasa beni hiyo inaangalia ni sekta ipi yenye mwelekeo wa kukopesheka.

“Kipindi hiki ni cha mpito bado watu hawajatulia, tunaangalia ni sekta ipi yenye mwelekeo kwa sababu kama hoteli zinayumbayumba lazima tusubiri hali ikae vizuri.

“Sisi tunasimamia fedha za watu hivyo hatuwezi kucheza nazo, tunazidi kujipanga kufuatana na sera ya Serikali,” alisema Dk. Kimei.

Akitoa mfano,   alisema sekta za mafuta na gesi ni kama vile zimesimama hivyo CRDB inasubiri hali ikae vizuri iweze kufanya tathmini.

“Mikopo mingine kama ya watu binafsi tunaendelea kuitoa na kama ni waajiriwa waje watapewa lakini katika sekta nyingine hali imekuwa tete sana,” alisema.

Serikali ilieleza kuwa miongoni mwa maeneo ya vipaumbele yatakayozingatiwa kama yalivyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17 ni pamoja na kuendeleza huduma za fedha, biashara na masoko.

Hata hivyo, hatua ya Serikali kutangaza mkakati wa kupunguza na kuondoa matumizi yasiyo ya lazima imeanza kuathiri sekta nyingi ikiwamo ya fedha.

Licha ya mkakati wa kubana matumizi, pia Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika ada ambazo benki inatoza wateja wake kwenye huduma mbalimbali zinazotolewa ni miongoni mwa  vitu vilivyochangia mtikisiko huo.

Wakati akisoma bajeti ya serikali bungeni kwa mwaka 2016/17, Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango, alisema serikali inakusudia kutoza VAT katika huduma za  benki zinazotozwa na benki zote nchini ili kupanua wigo wa kodi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles