27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Kikwete awataka wawekezaji kuja kuwekeza nchini

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

RAIS mstaafu Dk. Jakaya Kikwete amesema maonyesho ya 47 yanatoa fursa kwa wafanyabiashara kutangaza bidhaa zao na wawekezaji kuja kuwekeza nchini.

Amesema fursa hiyo si kwa wafanyabiashara pekee ila ni Watanzania wote kuonesha fursa mbalimbali zilizopo nchini kwa lengo la kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kwa Taifa.

Dk. Kikwete ameyasema hayo Julai 6, 2023 baada ya kutembelea maonyesho hayo ya Sabasaba yanayohusisha wafanyabaishara wa ndani na nje ya nchi ambao wakikaa pamoja wanabadilishana mawazo ya kibiashara na kuleta ufanisi ndani ya nchi zao.

“Wafanyabiashara wakikaa pamoja ni lazima watabadilishana uzoefu kujua huyu anafanya nini na yule anafanya nini hivyo kwa kupitia maonyesho haya najua yataleta tija nchini,” alisema Dk. Kikwete.

Dk. Kikwete alisema kwasasa Serikali inatafuta wawekezaji nje ya nchi ili waje kuwekeza nchini hivyo kama wamefika nchini Kuna umuhimu mkubwa wa kuwashawishi ili waje kwa wingi kuwekeza.

Hivyo, wataalamu wa uwekezaji watumie lugha sahihi na kuwatangazia fursa zilizopo nchini ili wawekezaji hao waje kwa wingi.

“Leo nimetembelea zĂ idi mabanda ya wafanyabiashara wa nje na nimewauliza ni lini wanakuja nchini kujenga viwanda wameniambia wataanza proces za uwekezaji hivi karibuni ni meona hiko ninkitu kizuri kwetu,” alisema Dk. Kikwete.

Dk. Kikwete alisema alisifia maonyesho hayo na kusema kuwa ni mazuri na yamekuwa yakiimarika kila mwaka.

Akizungumzia vyuo vikuu vilivyopo nchini alisema ni muhimu kuendeleza rasilimali watu ili kupata watendaji wazuri ndani ya nchi.

Alisema rasilimali watu inajengwa na Elimu Bora na vyuo vilivyopo nchini hivi sasa vinajitahidi kutoa elimu bora kwa wanagunzi.

Alisema Tanzania ni nchi ya Viwanda hivyo kunatakiwa kupatikana kwa rasilimali Bora ili waweze kufanya kazi kwa bidii na kukuza uchumi wa nchi.

“Nimepitia katika mabanda ya vyuo kadhaa nimeiona bunifu wanazozitengeneza hivyo nimeiona mambo si mabaya kwa sababu tukitumia vizuri rasilimali watu uchumi wa nchi utakuwa na Taifa litaongeza Pato lake,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles