21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Kijaji: Maonyesho ya Sabasaba ni lango la fursa kwa Watanzania

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashanti Kijaji amesema Maonesho ya 47 ya Sabasaba yamekuwa ya mfano wa kuigwa tofauti na miaka mingine iliyopita kwani sasahivi kumpuni nyingi za nje na ndani zimeshiriki.

Dk. Kijaji amebainisha hayo leo Julai 4, 2023 jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea mambanda tofauti yaliyopo kwenye maonyesho hayo akiwa na viongozi mbalimbali.

Amesema zaidi ya kampuni 3,000 za Kitanzania na 2,666 za nje zimeshiriki maonyesho hayo hali inayopechochea kukuza ushirikiano wa kibiashara miongoni mwa nchi zilizoshiriki.

“Kukutana kwa kampuni hizi kushiriki kwa wingi yatasaidia kampuni za Tanzania kupata uzoefu kutoka katika kampuni hizo hali itakayosaidia kuendeleza kampuni zao kisasa na kuongeza uzalishaji,”amesema Dk. Kijaji.

Amesema licha ya kampuni za ndani kupata ujuzi pia maonesho hayo yanafungua fursa kwa wawekezaji kuja nchini kuwekeza katika sekta mbalimbali.

“Naamini maonesho haya ya 47 yataleta tija kwa kuwakaribisha wawekezaji wengine kuja nchini kuwekeza,” amesema Dk. Kijaji.

Amesema zimeingia kampuni zaidi ya 150 kutoka nchini China kwa kutumia usafiri wa Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL) kwa ajili ya kuja kutembelea maonyesho haya.

“Hilo ndilo Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan amesema anataka kufungua nchi na kuufunganisha uchumi kwa shughuli zetu tunazofanya na ndiyo hili linaloendelea kutokea,” amesema Dk. Kijaji.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwenye maonyeshohayo yanayoendelea hadi JUlai 13, mwaka huu ili kujifunza na kupata fursa za kibiashara kutoka kwenye kampuni za ndani na nje ya nchi.

Dk. Kijaji pia amesema kutakuwa na makongamano mengi ya biashara ambayo yatatoa elimu na fursa za kibiashara wakati wa maonyesho na baada ya maonyesho ambapo kutakuwa na siku ya Irani, China na siku ya India kwa biashara pia kutakuwa na siku ya ambapo siku hizo zitatangaza fursa zipatikanazo kwenye nchi hizo huku viongozi wakuu wa nchi hizo wakishiriki kwenye makongamano hayo.

“Wafanyabiashara wa Kitanzania tuendelee kuboresha na kubuni bidhaa nzuri kwa sababu wateja wapo na wanazipenda Kwani nimeudhulia maonyesho ya biashara china nimeona wakiylizia bidhaa zetu hata kuzinunua,” amesema Dk. Kijaji.

Naye, Katibu Mkuu wa Chama cha RPF Inkotanyi wa nchini Rwanda, Komredi Wellars Gasamagera amesema katika maonesho hayo kuna wafanyabiashara kutoka nchini Rwanda ambao wamefika kuonesha bunifu zao mbalimbali.

“Tunashirikiana na nchi ya Tanzania katika mambo mengi ikiwemo no kubadilishana ujuzi wa biashara ili kukuza umoja na ushirikiano wa nchi zetu,” amesema Ngasamagera.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles