28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Dk. Kebwe aagiza wananchi wahame Mto Kilombero

Na ASHURA KAZINJA-MOROGORO

MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Stephen Kebwe, amewataka wakazi wa Kijiji cha Ngombo, kilichopo Wilaya ya Malinyi, mkoani hapa, kuanza kuondoka eneo hilo oevu la Mto Kilombero ili kufanikisha mradi wa kufua umeme katika Mto Rufiji.

Dk. Kebwe alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki wakati wa ziara yake wilayani Malinyi ambapo pia alitembelea eneo la kijiji hicho ambalo lipo ndani ya Bonde la Mto Kilombero.

Alisema kwamba, eneo hilo ni chanzo cha maji cha  Mto Kilombero ambao unachangia asilimia 65 ya maji yote ya Mto Rufiji ambao unatazamiwa kuendesha mradi wa kufua umeme chini ya mradi wa Stieglers Gorge.

“Kuanzia leo, muanze kuondoka na kurudi kwenye maeneo yenu mliyotoka, japokuwa ninajua wengi wenu mmetoka Malinyi na wengine Kilombero.

“Rudini kwenye maeneo yenu kwa sababu eneo mlilomo tunataka kuzalisha umeme kwa ajili ya maendeleo ya Taifa na hatuwezi kuwaacha muendelee kuishi kwa sababu mnaishi katika maeneo mliyomo kimakosa,” alisema Dk. Kebwe.

Pamoja na hayo, alisema wananchi wana nafasi ya kuhifadhi Bonde la Mto Kilombero kwa ajili ya mradi huo wa umeme ili kuungana kwa vitendo na kauli ya Rais Dk. John Magufuli anayehimiza mara kwa mara uwepo wa viwanda nchini.

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Bonde la Kilombero, Linux Lewis, alisema bonde hilo lina umuhimu katika uhifadhi siyo tu kwa ajili ya kutekeleza mradi stieglers gorge bali pia kimataifa kwa ajili ya matumizi ya vizazi vijavyo.

“Bonde la Mto Kilombero ni muhimu sana katika maisha yetu ndiyo maana tunatakiwa kulinda kwa nguvu zetu zote,” alisema Lewis.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles