26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Hoseah: Uhusiano wa TLS na Serikali, Bunge umeimarika

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mgombea wa nafasi ya Urais katika Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS), Dk. Edward Hoseah amesema uhusiano baina ya chama hicho na mihimili ya Serikali na Bunge umeendelea kuimarika hatua inayowezesha kushauriana.

Dk. Hoseah ameyasema hayo leo Jumatano Mei 11, 2022 jijini Dar es Salaam huku akisisitiza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu amefungua milango ya kusikiliza.

“TLS tumezidi kuimarisha mahusiano yetu na Bunge, pale TLS kuna Kamati ya Katiba na Sheria kila mswada unaoletwa na Serikali sisi tuna uchambua ili kuishauri Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge na mambo yamekuwa yakienda vizuri.

“Kwenye kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan amefungua milango ya kusikiliza, tulipata nafasi ya kukutana naye na tulimshauri azingatie Utawala wa Sheria,” amesema Dk. Hoseah na kuongeza kuwa:

“Moja ya mambo ambayo nimeshiriki kuyafanya nikiwa Rais wa TLS tuliandaa Kitabu Maalum, ambacho tulimshauri Waziri wa Habari juu ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, na mnamkumbuka mwanzoni Waziri wa Habari alikua na Mamlaka makubwa san,” amesema.
Kuhusu kujihusisha na siasa amesema kuwa chama hicho hakipaswi kujihusisha na mambo hayo.

“Miongoni mwa mambo ambayo TLS hatutakiwi kujihusisha nayo ni siasa, ndiyo maana mimi huoni nikitoa matamkoa kuhusu vyama vya siasa, nahitajika kuwa katikati,” amesema Dk. Hoseah.

TLS kinatarajia kufanya uchaguzi Mkuu katika nafasi ya Rais, Makamu wa Rais na Mweka hazina.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Mei 27, mwaka huu jijini Arusha, ambapo tayari kampeni za wagombea urais zimeanza tangu Aprili 15 na zinatarajiwa kuhitimishwa Mei 26, mwaka huu siku ambayo pia utafanyika uchaguzi katika nafasi nyingine ukiwamo ya viongozi wa kanda.

Uchaguzi huo ni kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ambao hufanyika kila baada ya mwaka mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles