29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Gwajima: CT SCAN zitasambazwa Hospitali za Rufaa na Wilaya nchini

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Doroth Gwajima amesema Serikali ipo katika hatua mbalimbali kufunga vipimo vya CT Scan katika Hospitali zote za Rufaa za Mikoa na baadhi ya Halmashauri.

Akizungumza leo Oktoba 28,2021,wakati wa uzinduzi wa huduma ya upimaji UVIKO-19 kwenye maabara ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Waziri Gwajima amesema serikali ipo katika hatua mbalimbali kufunga vipimo vya CT Scan katika Hospitali zote za Rufaa za Mikoa na baadhi ya Halmashauri.

“Hii ambayo tunasema CT Scan  mpaka mtu abebwe katika gari huduma nyingi zinaimarishwa MRI nazo zinaendelea kununuliwa,ipo mipango pale Wizarani na kuna fedha  zimeelekezwa katika Hospitali za rufaa tunataka kuonesha mipango yetu kwa wananchi,”amesema Dk. Gwajima.

Gwajima amesema serikali ya awamu ya sita inajielekeza kusukuma huduma ya upimaji wa UVICO 19  karibu na wananchi katika Mikoa yote Tanzania ndio maana imeanza kutoa huduma za upimaji mkoani Dodoma.

Amesema huduma ya upimaji wa UVIKO 19 kwa Mkoa wa Dodoma  ilianza Augost 26 mwaka huu ambapo jumla ya sampuli 839 zimeishapimwa ambapo amedai 343 ni za wakisiwa na 493 ni za wasafiri.

“Kuanzishwa kwa huduma hii kumesaidia kupunguza muda wa kusubiri sasa wanasubiri kwa saa tatu hii ni hatua kubwa na imeondoa gharama ya kusafirisha vipimo kutoka Dodoma mpaka Dar es salaam. Nitumie nafasi hii kuwaalika wadau wa maendeleo kuanzisha huduma kama hii ndugu wadau karibuni vita ya Uviko 19 hii  ni vita ya dunia,”amesem.

Kwa upande wake,Katibu  Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Profesa Abel Makubi ameliomba Shirika lisilokuwa la Kiserikali linalotekeleza afua za miradi ya afya (MDH) kutengeneza maabara zenye kutoa vipimo vyenye ubora kwani katika eneo hilo bado kuna changamoto ya ubora.

“MDH niwaombe mambo mawili la kwanza kusapoti mifumo ya maabara bado tuna changamoto ya Quality katika maabara.Kuendelea kusapoti suala la chanjo kwani bado tuna safari kubwa hasa katika suala la elimu,”amesema.

Kwa upande wake,Mtendaji Mkuu wa Shirika lisolokuwa  la Kiserikali linalotekeleza afua za miradi ya afya (MDH),David Sando amesema Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto iliamua kugatua huduma za upimaji za UVIKO 19 kutoka Maabara Kuu ya Taifa kwenda katika Mikoa ya Mwanza,Dodoma na Arusha.

Amesema lengo kuu ni kusogeza huduma kwa waathirika wa UVIKO 19 ili waweze kupata huduma hiyo kwa ukaribu kupitia kanda zote.

“Utekelezaji wa mpango huu ni moja ya maazimio ya mapango wa Taifa wa usalama wa afya wa 2017-2021 kwa kutumbua juhudi za makusudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita MDH imeamua kuongeza vituo vitatu vya Mwanza,Arusha na Dodoma huduma hizi ni kwa ajili ya utambuzi wa vimelea  kwa kutumia njia ya vina saba,”amesema.

Amesema ili maabara hizo ziwe na ubora MDH imesaidia kukarabati maabara hizo na kwa Mkoa wa Dodoma wameweza kutengeneza dirisha dogo kwa ajili ya viongozi wandamizi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles