29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Dk Bokhary: Lishe duni husababisha mapacha walioungana

 AVELINE KITOMARY – DAR ES SALAAM

DAKTARI bingwa wa upasuaji kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Zaituni Bokhary amesema lishe duni na akinamama kutokuhudhuria kliniki ipasavyo huweza kusababisha watoto mapacha kuzaliwa wakiwa wameungana.

Akizungumza na MTANZANIA mwishoni mwa wiki hii, Dk Bokhary alisema ukuaji mzuri wa mtoto hutegemea hali ya afya ya mama mjamzito hivyo ni vyema akinamama wakazingatia lishe bora kabla hata ya ujauzito. 

“ Tunapoongelea mapacha walioungana, hawa ni watoto wanaozaliwa hali ya kuwa wameungana, huwa hakuna sababu maalumu lakini kinachotokea katika hali hii ni kwamba lile yai ambalo limerutubishwa kwa mwanamke linakuwa linaungana kama kujiandaa kutengeneza mapacha.

“Kwa hiyo badala ya yai moja kurutubishwa yanakuwa mawili ili kutengeneza mapacha. Jinsi mimba inavyoendelea kukua, tunaamini kuwa mama akiwa anahudhuria kliniki vizuri atapata vitu muhimu ambavyo mama mjamzito anategemea kupata, ikiwemo ushauri wa vyakula vyenye mlo kamili na madini anayotakiwa kutumia ili mtoto azaliwe akiwa timilifu.

“Lakini mara nyingi akinamama ambao hawatumii madini kama folic acid au vyakula bora, wale wanaotapika sana matokeo yake ni kuzaa mtoto mwenye hitilafu. Pia ni sababu zinazochangia watoto kuzaliwa wakiwa wameungana kwa sababu kuungana ni hitalifu ambayo mtoto anaipata akiwa tumboni,”alisema Dk. Bokhary. 

 Alisema watoto wanapondelea kukua wakiwa katika tumbo la uzazi wakiwa wameungana kuna uwezekano wa kutenganishwa au kutokutenganishwa kulingana na sehemu walizoungana.

“Watoto wanaweza wakaungana sehemu ya kichwa, kifua,tumbo, nyonga na sehemu zingine hivyo nafasi ya hawa watoto kutenganishwa ipo, lakini inategemea wameungana sehemu gani za mwili. Kuna sehemu muhimu sana kama vile sehemu za kifua ambako kuna moyo kama wanachangia moyo inaakuwa vigumu kuwatenganisha kwahiyo inabidi waachwe wakiwa katika maumbile hayo ,” alieleza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles