25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Dk. Biteko kushiriki uapisho wa Rais mpya Botswana

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko anaiwakilisha Serikali katika sherehe za uapisho wa Rais Mteule wa Botswana Gideon Duma Boko zitakazofanyika Katika Uwanja wa Taifa wa nchi hiyo Novemba 8, 2024.

Akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Gaborone, Dk. Biteko amepokelewa na Katibu Mkuu wa Vijana, Jinsia, Utamaduni na Michezo, Bridget John, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James Bwana pamoja na maafisa wengine waandamizi wa Nchi hiyo.

Gideon Duma Boko ni Rais wa Sita Botswana kupitia chama cha Umbrella for Democratic Change.

Uchaguzi Mkuu nchini Botswana ulihitimishwa Oktoba 30, 2024 ambapo Rais Mteule Gideon Boko aliibuka mshindi katika uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles