29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Abbas azikumbusha Basata, Cosota kutokuwa kikwazo kwa Wasanii

Na Brighiter Masaki, Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Hassan Abbas, ameitaka Taasisi za Sanaa(BASATA na COSOTA) kutumika katika kuendeleza sanaa na sio kuwa chombo cha kukandamiza wasanii.

Akizungumza na wasanii Alhamisi Juni 24, 2021 jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri Innocent Bashungwa, kwenye ufunguzi wa jukwaa la elimu ya masoko na mabadiliko ya matumizi ya Kidigital kwa kazi za muziki, nchini lililoandaliwa na Kampuni ya Transsnett Music Tanzania (Boom play Artister Forum)

“Taasisi zetu zinatakiwa ziwe sehemu ya kukuza sanaa na sio kugeuka kuwa Polisi ama mgambo kukamata kazi za wasanii, tuzingatie kazi za sanaa na kuwasaidia wasanii, kukuza sanaa zao na sio kuwakandamiza.

“Niwakati wa wasanii kufanyakazi bora kwakuwa jamii imekubali sanaa yao, wasanii tumieni vipawa vyenu na ubunifu kufanyakazi na kujua jinsi ya kuziuza kazi zenu kwa kutumia Boom Play,” amesema Abbas.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa Serikali chini ya Rais Samia Suluhu, mwishoni mwa mwaka huu itaanza kutoa mirabaha kwa wasanii,

“Niwahakikishie kuwa serikali ipo tayari kushirikiana na wasanii na kuboresha kazi zao, na kutumia njia tofauti katika kukuza kazi zao, kutumia mitandao mbalimbali,” amesema Dk. Abbas.

Kwa upande wake Meneja wa Boom Play Tanzania, Natasha Stambul, amesema wapo tayari kushirikiana na serikali katika kusaidia wasanii kwa kuweza kukuza kazi zao kwa kutumia mitandao mbalimbali kwakuwa Tanzania kunawatumiaji milioni 11, hivyo wanaowezo wa kuwafikia watu wengi kwa haraka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles