23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

Mkandara Barabara Mwigumbi – Maswa atii agizo la Kafulila

Na Derick Milton, Simiyu

Siku chache baada ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu, David Kafulila, kuzuia malipo kwa Mkandarasi CHICCO anajenga barabara ya Mwigumbi mkoani Shinyanga hadi Maswa Mkoani Simiyu kutokana na kujenga chini ya kiwango mradi huo na kuagiza arudie, mkandarasi huyo ameanza utekelezaji wa agizo hilo.

Mtanzania Digital imeshuhudia Mkandarasi huyo akiwa eneo la kazi akiendelea na utekezaji wa agizo hilo la kurudia ujenzi wa barabara hiyo kwenye maeneo yote ambayo yameanza kuharibika kutokana na kujengwa chini ya kiwango.

Aidha, mkandarasi huyo ameanza kufunga kwa kamba maeneo yote ambayo yameharibika na kuzuia magari kupita huku akitengeneza barabara mbadala (Division Road) kwa ajili ya magari kupita ambapo maeneo mengine ameanza kutengeneza Barabara hizo mbadala.

Aidha, imeshuhudiwa Mkandarasi huyo katika maeneo ambayo amefunga barabara kwa ajili ya kurudia ujenzi, vifaa vyake vimeonekana vikiondoa rami nzima iliyokuwepo na kuanza kuweka rami nyingine mpya.

Ikumbukwe kuwa mara baada ya kuapishwa na kuwa Mkuu wa mkoa huo, Kafulila kazi yake ya kwanza ilikuwa kufanya ukaguzi kwenye barabaray hiyo ambayo ilikuwa imeharibika zaidi na kubaini kuwa imejengwa chini ya kiwango.

Jambo ambalo lilimshangaza zaidi Mkuu huyo wa mkoa, ni kuanza kuharibika kwa barabara hiyo ambayo imegharimu zaidi ya Sh bilioni 60, lakini imeanza kuharibika kabla ya ujenzi kukamilika lakini pia kabla haijafunguliwa.

Wakiongea na Mtanzania Digital baadhi ya wananchi na madereva wanatumia barabara hiyo wamempongeza mkuu huyo wa mkoa wakati akikagua aliagiza ujenzi urudiwe.

“Nadhani hii barabara ilimsubiria huyu mkuu wa mkoa, maana imeanza kuharibika muda mrefu na yeye kabla hajateuliwa, lakini viongozi na wataalamu walikuwepo, bila ya Kafulila kodi zetu wananchi zilikuwa zimeliwa,” amesema Joas Jamila ambaye ni dereva.

Kwa mujibu wa Meneja wa Tanroads Mkoa, Mhandisi Albert Kent, Mkandarasi huyo anarudia ujenzi huo kwa gharama zake mwenyewe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles