29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 5, 2024

Contact us: [email protected]

Diwani Rorya alia na ufisadi TARURA

*Asimulia mbele ya wananchi Milioni 400/ za daraja zilivyopigwa na wajanja, Mbunge aguswa

Na Mwandishi Wetu, Mara

DIWANI wa Kata Nyathorogo Halmashauri ya Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Dalmas Nyagwal, ameweka wazi namna wajanja wachache ndani ya Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) wilayani hapa walivyokwamua kiasi cha Sh milioni 400 za ujenzi wa Daraja kubwa la kata hiyo.

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa msimamo wake umemfanya kuchukiwa na baadhi ya viongozi wenzake wa kisiasa jambo ambalo haitamfanya arudi nyuma kwa maslai ya wananchi wake.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika mwishoni mwa wiki, uliofanyika katika eneo la Kumbini Kata ya Nyathorogo, amesema hatua ya kukwamishwa kwa ujenzi huo ni mkakati wa makusudi na mtandao wa wizi wa fedha za miradi ya Serikali.

Kutokana na hali hiyo amesema licha ya fedha za Serikali kutumika kiholela lakini ni vea mamlaka husika zikaedelea kuchukua hatua na fedha hizo za Serikali zilirudishwe zikafanye kazi iliyokusudia ili kuwaondolea adha wananchi.

“Kwa sababu fedha za Serikali zina utaratibu wake, mimi ninachohitaji ni maendeleo ya wananchi wangu kwa hiyo niliendelea kusubiri mkandarasi afanye kazi ikiwamo kutangaza tenda, basi afanye kazi ya kujenga daraja.

“Muda ulivyozidi kwenda kabrasha la kwanza nikaandikiwa milioni 400 na la pili 350 nikauliza imekuaje hii fedha inashuka wakati hakuna kinachoendelea kufanyika kwenye ujenzi wa daraja. Majibu nikaambiwa ni kwamba unaweza kuomba milioni 400 lakini zikaingizwa kwa awamu hivyo tumepokea milioni 350.

“Nikasema sawa nikaendelea kusubiri nione nini kinafanyika, mimi naita wana Nyathorogo ni usanii wakaenda kutafuta mainjiania wengine tofauti na wale waliofanya usanifu mwanzoni ambao walisema wakipata milioni 500 daraja linapitika.

“Wakaja na mainjinia wengine wakasema wanataka bilioni 1.1, hapo ndipo ilipoanzia shida, kumbukeni yule wa kwanza alikuja akasema tukipata milioni 500 daraja linapitika, lakini bahati nzuri si kama walihama wale waliofanya usanifu mwanzoni ila waligeuka na kusema wanataka bilioni 1.1 nikasema basi anzeni na hizo milioni 350 zilizopo hata kwa kujenga msingi,” amesema Diwani Nyagwal.

Akieleza kuhusu sakata hilo, Diwani huyo alisema kuwa jambo hilo lilichukua muda ambapo kufika mwaka 2022 Julai akiwa safarini kuelekea mkoani Mwanza, alipogiwa simu na Mbunge wa Rorya Jaffari Chege, akimtaka wajadili kuhusu fedha za daraja.

“Ninaongea nanyi kwa sababu nyie ndiyo mmenituma, zile fedha ambazo mmepewa kwa ajili ya Daraja la Nyathorogo ni kama tunahitaji fedha zaidi. Hivyo Mbunge akanitaka nibadili matumizi ili tujenge barabara, nikamjibu hapana maana niliona hili si sahihi kwa wananchi ambao wanahitaji daraja maana nitaonekana nimevunja uamivu kwa jambo kubwa kama lile.

“Nilipokataa akaniambia niongee na Injiani Abas, kesho yake nifanya hivyo na nikamuliiza kama aliongea na Mbunge akaniambia ndiyo tunataka mbadili fedha za matumizi ya daraja, nikasema hapana naombeni kwa fedha iliyokuwepo hata kama msingi jengeni.

“…kwa hiyo kwenye hilo nikamwambia injini hatutoelewa, ilipofika mwezi wa sita au Saba nikapata safari ya kwenda Kyerwa mkoani Kagera siku moja nikapigiwa simu na Bwana moja akaniambia habari ya siku Mheshimiwa, nilipata habari zako ulivyomkatalia Mbunge zile fedha zisiondeke lakini sasa zile fedha zimeondoka, nikampigia simu DC nikamwambia kuwa TARURA wameondoa fedha kwa ajili ya daraja kitu ambacho mimi hakitaniletea usalama wa kiafya kwenye siasa za kata yangu,” amesema.

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa ilipofika kweye Bajeti ya Mwaka 2022/23 alikwenda kuzungumza kwenye kikao cha Baraza ambapo ilimlazimua kuwaalika wananachi ili wakasikia hatima ya ujenzi wa daraja hilo.

“Tukaenda kwenye Baraza la TARURA na bahati nzuri mbunge alikuwepo na nikazungumza kuwa fedha za daraja zimeondolewa, alisimama na akakiri kuwa zile fedha zilikuwa hazitoshi kwamba kuna barabara imetoka Utegi kwende Nyasoko, baada ya mimi kuweka wazi hili limetengezea vita kwenye siasa na hata kuniweka mbali na mbunge.

“Na katika hili alitumika diwani mmoja waliniita hadi Musoma ili wanihonge nikagoma na baadae yule Injinia wamemuhamisha yupo Singida, kazi ya Diwani ni ngumu sana ndugu zangu,” amesema.

Kutokana na hali hiyo alipotafutwa Meneja wa TARURA Wilaya ya Rorya, Elifadhili Moses amesema suala hilo kwake ni geni na kuoba kulifanyika kazi zaidi.

“Mimi nimeripoti hapa Rorya Januari mwaka huu, hiyo ni lazima nianze kuangalia taarifa zote za nyuma ili niweze kubaini suala hilo kwa undani. Hivyo ninaomba nilifanyie kazi kwanza ndugu yangu,” amesema Meneja huyo wa TARURA.

Hata hivyo alipotafuta Mbunge wa Rorya kwa simu yake ya mkononi , hakupatikana na tunaendelea kumtafuta ili kupata ufafauzi wa sakata hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles