24 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Diwani Athuman DCI mpya

athumanNa Elias Msuya, Dar es Salaam
RAIS Jakaya Kikwete amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Diwani Athumani Msuya kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI),.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, kabla ya uteuzi huo, Diwani alikuwa Kaimu Kamishna wa Kamisheni ya Intelijensia ya Jinai.
“CP Diwani anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Robert Manumba ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria,” inasema taarifa hiyo.
Akizungumzia uteuzi huo, Diwani, alisema matarajio yake ni kuona Tanzania inaendelea kuwa na amani, utulivu na usalama.
“Namshukuru Mungu, Rais na uongozi wa Wizara, IGP, makamishna na wengine kwa namna tunavyoshirikiana kazi hadi sasa.
“Umoja wetu ndiyo nguzo kubwa. Matarajio makubwa ni kuendelea kuiona nchi yangu Tanzania ikiendelea kuwa na ya amani, yenye utulivu na usalama.
“Kila Mtanzania awe na mchango katika suala la kulinda usalama ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu,” alisema Diwani.

Rais Kikwete pia amemteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Valentino Mlowola kuongoza Idara ya Intelijensia ya Jinai, kujaza nafasi inayoachwa na Diwani.

“Kabla ya uteuzi huu, Mlowola alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza. Uteuzi huo umeanza Mei 3 mwaka huu,” ilisema taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles