25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Diouf aitoa Liverpool ubingwa England

LIVERPOOL, ENGLAND

NYOTA wa zamani wa timu ya Liverpool, El Hadji Diouf, amefunguka na kusema itakuwa ngumu kwa timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu bila ya kujali kuanza vizuri katika michezo yake.

Kwa sasa Liverpool inaongoza kwenye msimamo wa Ligi huku ikiwa na pointi 18 baada ya kushinda michezo yote sita, wakifuatiwa na mabingwa watetezi wa michuano hiyo Manchester City wenye pointi 13.

Mchezaji huyo anaamini kiwango ambacho walikionesha Liverpool msimu uliopita kilikuwa cha hali ya juu na walistahili kutwaa ubingwa, lakini msimu huu itakuwa ngumu kupambana kama ilivyo msimu uliopita.

“Sioni kama Liverpool wanapambana kama ilivyo msimu uliopita, walikuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa dhidi ya Manchester City, taji lilikuwa mikononi mwao lakini walilala na kuwaachia City.

“Kabla ya kufika wakati wa Krismasi walikuwa wanaongoza kwa pointi saba, lakini kitu cha kushangaza ni kwamba Man City waliweza kupambana na kufanikiwa kuwa mabingwa kwa tofauti ya pointi moja.

“Kama waliweza kumaliza ligi msimu uliopita kwa tofauti ya pointi moja sidhani kama wataweza kufanya hivyo tena, hiyo ni sawa na kutwaa ubingwa, lakini msimu huu watakutana na changamoto kubwa ambazo haziwezi kufanana na msimu uliopita.

“Mbali na Man City kuanza vibaya, lakini ninaamini wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri tena kwa mara ya tatu mfululizo,” alisema mchezaji huyo.

Diouf alijiunga na Liverpool mwaka 2002 na akaja kuondoka 2005 huku akiwa amecheza jumla ya michezo 79 na kupachika mabao sita, amedai aliondoka kutokana na kunyanyaswa, lakini bila hivyo anaamini angekuwa mmoja kati ya wachezaji bora duniani.

Lakini mchezaji huyo raia wa nchini Senegal, alifanikiwa kuwa mchezaji bora Afrika mara mbili, alitangaza kustaafu soka mwaka 2015.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles