Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini na kiongozi wa kundi la WCB, Naseeb Abdul ‘Diamond’, amefanikiwa kushinda tuzo ya mwimbaji bora wa kiume Afrika Mashariki mwaka 2017 nchini Uganda.
Tuzo hizo ambazo hutolewa nchini humo kila mwaka na kushindanisha wasanii mbalimbali, zilifanyika Jumamosi iliyopita, huku msanii mwingine wa kundi la WCB, Raymond ‘Rayvanny’, akipata tuzo ya mwimbaji bora wa kiume Afrika mwaka 2017.
Mbali na kuibuka na tuzo hizo, Diamond ameendelea kufanya vizuri, baada ya kupata nafasi ya kuwa balozi wa kinywaji maarufu duniani cha Luc Belaire.
“Nashukuru mashabiki zangu wote duniani wameonyesha jinsi gani kila kitu kinawezekana kwa kufanikisha ushindi wangu katika tuzo hizo,” aliandika Diamond kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram