30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Diamond Platnumz ndio habari ya mjini

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul 'Diamond' akiwa na tuzo yake akizunguka mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam baada ya kuwasili jana akitokea Marekani
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul ‘Diamond’ akiwa na tuzo yake akizunguka mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam baada ya kuwasili jana akitokea Marekani

NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasseb Abdul ‘Diamond’, jana amesherehekea tuzo yake ya Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki ya AFRIMMA kwa kupita mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam hadi nyumbani kwao alikokulia, Tandale.

Katika eneo hilo kulikuwa na muziki kwa ajili ya burudani ya kumpokea Diamond, aliyezunguka Kariakoo, Tandale na kumalizia nyumbani kwake Sinza.

Msafara wa Diamond ulipambwa na shangwe kuanzia Tazara, ukiongozwa na pikipiki zilizoandaliwa kwa ajili ya kumpokea akiwa katika gari ya wazi na tuzo yake.

Akizungumza nyumbani kwake, Diamond alisema tuzo hiyo imemfundisha mambo mengi, ikiwa ni pamoja na kumuongezea kasi ya kufanya vema ili kujitangaza kimataifa.

“Hii ni changamoto kwangu, lakini pia na kwa wasanii wengine, tuzidi kujiimarisha na kufanya kazi zinazokubalika kimataifa ili kuitangaza nchi yetu,” alisema.

Naye mama yake Diamond alishindwa kuzungumza kutokana na furaha aliyonayo, huku akisema amefurahi kwa mafanikio ya mwanaye.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. jamani mimi ningependa wataanzania tuwe makini sana na hawa wanasiasa tuache ushabiki tuangalie chama chenye dhamira ya kweli kuikomboa tanzania, mimi naimani tukipata kiongozi bora hii nchi ni nzuri hakuna haja ya kufikiria kwenda ulaya, mambo ya ajabu ajabu watu wanapeana nafasi za kazi ina maana usipojulikana huna lako, hebu angalia zile tuhuma uhamiaji kama ni kweli basi ni aibu sana. sidhani katika watu wote ambao kwa namnamoja au nyingine walikuwa madarakani wakipewa madaraka kuna kitu watabadili nadhani sio rahisi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles