23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

DCEA yakamata wauzaji wakubwa wa dawa za kulevya na kuanzisha kanzidata

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Dk. Aretas Lyimo, ametangaza kukamilika kwa kanzidata ya wauzaji wakubwa wa dawa za kulevya na kuanza uchunguzi dhidi yao.

Akizungumza Julai 17, 2024, jijini Dar es Salaam, Kamishna Lyimo alisema mtuhumiwa Shabani Musa Adam (54) amekamatwa kwa kutengeneza heroin kwa kutumia dawa tiba za asili akichanganya na kemikali bashirifu. Adam alikamatwa Manzese Kilimani Juni 11, 2024, na alikiri kutengeneza dawa hizo nchini Asia na Tanzania.

Kamishna Lyimo pia alitangaza kukamatwa kwa Mbaba Rabini Issa, Mtanzania mwenye pasipoti namba TAE442718B, akiwa na kilogramu 3.8 za skanka katika uwanja wa ndege wa Melchior Ndadaye, Bujumbura, Burundi, akijiandaa kusafiri kuelekea Dubai.

“Ukamataji wetu unafanyika kufuatia mikataba ya kikanda na kimataifa iliyosainiwa na Tanzania kwa udhibiti wa dawa za kulevya,” alisema Lyimo, akisisitiza kuwa mhalifu yeyote wa dawa za kulevya atakayefanya uhalifu na kukimbilia nchi nyingine atakamatwa na kuchunguzwa.

Operesheni za DCEA katika mikoa ya Dodoma, Mwanza, Mtwara, na Mbeya zimefanikisha kukamata gunia 285 za bangi kavu, kilogramu 350 za dawa mbalimbali za kulevya, milimita 115 za dawa tiba za asili ya kulevya, na lita 16,523 za kemikali bashirifu. Watuhumiwa 48 walikamatwa katika operesheni hizi.

Profesa Mohamed Janabi, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), alisema hospitali hiyo inahudumia watu 3,840 walioathirika na dawa za kulevya, ambapo takribani watu 900 wanapokea methadone kila siku. Janabi aliongeza kuwa matumizi ya dawa za kulevya huathiri mfumo wa umeme wa moyo na kusababisha vifo vya ghafla.

DCEA inatambua na kuthamini ushirikiano wa vyombo vya ulinzi na usalama, asasi, vyombo vya habari, na Hospitali ya Taifa Muhimbili katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya, na imewapa tuzo kama zawadi ili kuendelea na juhudi hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles