26.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

DCEA yakamata skanka kilo 1,815

Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imewakamata watu watano kwa tuhuma ya kukutwa na dawa za kulevya kilogramu 1,815 aina ya skanka ambayo ni aina bangi ya kusindika yenye kiwango kikubwa cha kemikali yenye sumu aina ya Tetrahydrocannabinol (THC).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 10, 2024 Jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali (DCEA),Aretas Lyimo, amesema watu hao wamekamatwa katika operesheni iliyofanyika Agosti 28, 2024 hadi Septemba 2, 2024 katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Amewataja watuhumiwa walikamatwa kuwa ni Richard Henry Mwanri (47) ambaye ni Mfanyabiashara na mkazi wa Mbezi Makonde Wilaya ya Kinondoni, Felista Henry Mwanri (70) mkulima na mkazi wa Luguluni Mbezi Wilaya ya Ubungo ambaye ni mmiliki wa nyumba zilipokutwa dawa za kulevya.

Kamishna Jenerali Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 10, 2024 Jijini Dar es Salaam

Watuhumiwa wengine ni Athumani Koja Mohamed (58) mfanyabiashara na mkazi wa Mkoa wa Tanga, Omary Chande Mohamed (32) dereva wa bajaji mkazi wa Buza pamoja na Juma Abdallah Chapa (36) mkazi wa Kiwalani.

Kamishna Jenerali Lyimo amesema kuwa katika operesheni hiyo pia wamekamata gari aina ya Mitsubishi Pajero yenye namba za Usajili T551 CAB pamoja na bajaji yenye namba za usajil MC 844 CZV.

“Mtuhumiwa Richard Mwanri amekuwa akipokea dawa za kulevya za kutoka nchi mbalimbali na kuziingiza nchini kwa usafiri wa magari zikiwa zimefichwa kwa kuchanganywa na bidhaa nyingine kasha kusambaza kwa wauzaji” amesema.

Amefafanua kuwa dawa ya kulevya aina ya skanka ni aina bangi ya kusindika yenye kiwango kikubwa cha kemikali yenye sumu aina ya Tetrahydrocannabinol (THC) ambayo inaweza kuharibu mfumo wa fahamu, akili na kusababisha magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo moyo, figo na ini. Matumizi ya skanka kwa wajawazito inaweza kusababisha madhara kwa motto aliye tumboni ikiwemo kuathiri maendeleo ya ubongo na kuzaliwa na uzito mdogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles