29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi ya wanandoa yaahirishwa tena, shahidi apewa amri kuendelea kufika mahakami

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imeahirisha kusikiliza kesi inayowakabili wanandoa wawili, Bharat Nathwan na Sangita Bharat, kutokana na mmoja wa watuhumiwa ambaye ni Sangita kuwa mgonjwa, hivyo kuachwa apiganie afya yake kwanza.

Akiwakilisha ombi la kuahirishwa kwa kesi hiyo, Wakili wa Upande wa Utetezi, Edward Chuwa alimuomba Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya kuahirisha kesi hiyo na kuipangia tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kwa upande wa shahidi, ombi lililokuja kwa maelezo ya kuwa afya ya mteja wake haiko sawa, jambo ambalo lilikubaliwa na wakili wa upande wa mashtaka, Wakili Faraja Nguka ambapo amesema ugonjwa ni jambo nyeti na binafsi zaidi hawewazi kuwa na pingamizi juu ya ombi hilo.

Akitoa uamuzi wa maombi hayo, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Aaron Lyamuya alikubaliana na maombi ya wakili wa upande wa utetezi na kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 26,2024 itakapotajwa na kusikilizwa tena.

Katika hatua nyingine, Hakimu Lyamuya ametoa onyo na amri maalum kwa shahidi wa upande wa mashtaka, Kondo Kondo kuhakikisha anafika bila kukosa siku ya kusikilizwa kwa kesi hiyo ili kutoa ushahidi wake.

Licha ya mmoja wa watuhumiwa anayetajwa kuwa na changamoto ya kiafya, Sangita Bharat kufika mahakamani hapo, wakili wa utetezi, Chuwa aliwasilisha nyaraka muhimu za kitabibu zenye vielelezo vya kuthibitisha kuugua kwa mteja wake, nyaraka ambazo zilikubalika kwa upande wa mashitaka.

Wanandoa hao ambao wanaishi Mtaaa wa Mrima, Kisutu jijini Dar es Salaam wanatuhumiwa kwa mashtaka manne ikiwamo kutoa lugha chafu, kosa walilotenda Julai 21, 2023 kinyume cha sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles