25.4 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

DCB yaboresha huduma za Kidigitali, yajivunia ufanisi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

BENKI ya DCB imetangaza maboresho mapya ya Kidigital kwa wateja wake lengo likiwa ni kuhakikisha mteja anapata si tu huduma bora bali zenye gharama nafuu kwa njia ya mtandao salama na haraka zaidi.

Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB, Zacharia Kapama(Kushoto) akizungumza na (Waandishi wa Habari* Hawapo pichani).

Hayo yamebainishwa na Dar es Salaam Agosti 3, 2021 na Mkurugenzi wa Biashara wa DCB, Zacharia Kapama ambapo amesema kuwa kwa sasa mteja akiwa na kifaa chochote kinachomwezesha kupata huduma za kibenki anaweza kukiamilisha miamala yake kwa urahisi zaidi.

“Uboreshaji huu wa huduma zetu za kibenki kwa njia ya kidigitali unaonyesha nia yetu ya kufanya benki yetu kuzidi kupiga hatua na kua chaguo namba moja kwa kila anehitaji huduma za kifedha nchini kwa haraka na gharama nafu.

“Lakini pia, lengo letu ni kuhakikisha mteja anapata si tu huduma bora bali nafuu, pia aweze kupata Huduma kwa njia ya mtandao hivyo kwa sasa ukiwa na kifaa chochote kama Simu, tableti unaweza kufanya muamala yoyote ile. Hivyo uboreshaji wa huduma za kibenki kwa njia ya kidigitali ni moja ya tukio jingine la kihistoria kwa benki yetu ya DCB katika kudhihirisha kwa dhati nia yetu ya kufanya mabadiliko katika benki yetu kuzidi kupiga mwendo na kuwachaguo namba mojakwa kila anayehitaji huduma za kifedha nchini,” amesema Kapama.

Amesema kuwa benki hiyo imeendelea kutoa uhuru kwa wateja wake katika kufanya miamala ambapo sasa hivi imekuja na kadi ya VISA inayomwezesha mteja kutoa pesa kwenye ATMs zote za Visa duniani.

“Mwanzo tulikuwa tunatumia mfumo wa ATMs za Umoja Switch lakini tumeongeza mfumo wa Visa hivyo tunaenda mbali zaidi kwa kutoa kadi za visa ili kuwarahisishia wateja wetu kuweza kupata huduma za kifedha mahala popote pale duniani akiwa tu nakadi yake ya DCB Visa CARD,” amesema Kapama.

Katika hatua nyingine Kapama amesema kuwa benki hiyo imeendelea kuboresha mtandao wake wa mawakala nchini kwa kuanzisha mawakala wakubwa wanaohudumia wateja bila kuhitaji kufika kwenyebmatawi ya benki huku ikisogeza huduma kwenye Manispaa zote za Jiji la Dar es Salaam.

“Awali tulikuwa na mfumo wa Mawakala 700 nchi nzima lakini sasa tunafanya maboresho kwa kuwa na mawakala wakubwa ambao watatoa huduma zitakazolingana karibu na za tawi, hii inamaana kwamba kwa sasa wakala atakuwa na uwezo wa kumsaidia mteja kupata taarifa ikiwamo za mkopo wake, pia tunaweka mawakala wakubwa kwenye hamashauri zote za Dar es Salaam. Pia kwa kutumia akaunti yako ya simu sasahivi unaweza kupata mkopo salary advance hivyo tunawahamasisha watanzania kujiunga na benki hii,” amesema Kapama.

Akizungumzia mafanikio ya benki hiyo, amesema kuwa: “Wakati tunazindua kampeni yetu ya DCB PESA mwaka 2018 tulikuwa na wateja 150,000 lakini sasahivi tumefikia wateja 200,000 hii ina maana kwamba wateja wanaendelea kuongezeka.

“Lengo la kwanza ilikuwa ni kuongeza idadi ya wateja jambo ambalo tumefakinikiwa kwa kiasi chake. Pia tumeweza kuwafikia wateja wetu nchi nzima. Mafanikio mengine ni mizania ya benki imekua kwa asilimia 50 kutoka Sh bilioni 130 hadi 200.

“Kuna baadhi ya maeneo tumeondoa kabisa tozo, hii ina maana kwamba ufanisi wa benki umekuwa ukiimarika,” amesema Kapama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles