25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

DC Simiyu apiga marufuku mkutano wa Chadema

Derick Milton, Simiyu



Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu, Festo Kiswaga, amepiga marufuku kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema), unaotarajiwa kufanyika Jumapili Oktoba 21, mwaka huu.

Mkuu huyo wa wilaya amesema ni marufuku kufanyika kwa mkutano huo Bariadi, kwani viongozi wake hawajatoa taarifa kuhusu huo mkutano kwa ajili ya kupewa kibali, lakini pia mkoa huo una ajenda ya maendelo na si siasa.

“Lakini pia, tarehe za kufanyika kwa mkutano huo kama wilaya na mkoa tutakuwa na ugeni mkubwa wa wiki ya maonyesho na Viwanda Vidogo Sido na atakuwepo Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa, hivyo hatutakuwa na uwezo wa kulinda mkutano wao.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, amesema ni kweli watakuwa na kikao Bariadi, lakini kikao hicho kitakuwa cha ndani, na kitahusisha wanachama na viongozi wa Kanda ya Serengeti na ni kikao maalumu kwa ajili maandalizi na kuweka mikakati ya uchaguzi ngazi mbalimbali za chama hicho.

“Kutokana na kanda hiyo ni lazima kifanyikie Simiyu, mkoa ambao uko katikati ya mikoa ambayo inaunda kanda hiyo, kama Mkuu wa Wilaya amepiga marufuku hicho kikao kisheria hayuko sahihi na hana mamlaka ya kufanya hivyo, wala hatuwezi kusitisha hicho kikao tutaendelea na maandalizi yake na kitafanyika,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles