Na Raymond Minja
Mkuu wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, Jamuhur William amebainisha kuwa hadi ifikapo mwaka 2022 atahakikisha kaya zote 59,152 za wilaya hiyo zina vyo bora na salama ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko.
Akizungumza kwenye kilele cha siku ya maazimisho ya usafi wa mazingira duniani ambayo kimkoa yalifanyika Tarafa ya Makangali, Kata ya Mbalamaziwa alisema Mufindi ni moja kati ya wilaya ambazo inafanya vyema katika usafi wa mazingira ikiwemo ujenzi wa vyoo bora na salama.
Amesema katika wilaya yake kumekuwa na kampeni ya ujenzi wa vyoo bora na salama ili kusaidia wananchi kujikinga na magonjwa ya kuhara yanayosababishwa na kula kinyesi .
Alisema kuwa mwaka 2012 wilaya hiyo yenye kaya (59,152 )29% ndiyo iliyokuwa na vyoo safi huku 2% ambayo ilikuwa haina vyoo kabisa .
“Lakini hivi sasa baada ya kupata hela serekalini na kutoa elimu ipasavyo, hivi ninavyoongea asilimia 79 ya kaya inavyoo safi na salama na asilimia 21 ina vyoo vya kati pia hatuana kaya hata moja ambayo haina choo kabisa, haya ni mafanikio makubwa,” alisema William.
William alisema hadi kufikia 2022 atahakika kaya zote zinakuwa na vyoo safi na salama huku akiwataka wanachi kuhakikisha kila mmoja anakuwa na choo safi na salama kwa ajili ya matumizi take na familia yake.
“Wilaya ya Mufindi ni moja kati ya wilaya inayopitiwa na barabara kuu hivyo watu wanaosafir wamekuwa na tabia ya kuchimba dawa porini sasa ili kuepuka magonjwa ya mlipuko kwenye wilaya yetu pia kwa kushirikiana na wadau wa mazingira tumejenga vyo bora eneo la Edetero ili wasafiri wetu waweze kupata huduma ya choo pale na kuachana na Tabia ya kuchimba dawa porini,” alisema William.
Hata hivyo jamhuri aliwaonya wadau wa mazingira hapa nchini kuendelea kushirikiana na serikali kutoa elimu ya kujikinga na magonjwa ya mlipoko, ikiwamo kujenga vyoo pembezo mwa barabara ili wananchi waishio pembezoni mwa barabara kuwa salama na kujikinga na magonjwa ya mlipuko .
Remiginius Sungu ni Afisa Miradi na usafi wa mazingira kutoka Shirika la Kuhudumia Watoto Ulimwenguni (UNICEF) ambapo alisema wao kama shirika wamekuwa wakishirikiana na taasisi mbalimbali kutoa elimu ya usafi wa mazingira ikiwemo kujenga vyoo bora ili watu wajikinge na mgonjwa ya mlipuko.
Alisema kuwa afya ya mwanadamu inategemeana na mazingira anayoishi hivyo wamekuwa wakitoa elimu ya kutibu maji kwa kutumia vidonge ili yawe safi na salama kwa natumizi ya binadamu.
“Nitoe woto kwa wananchi na hata taasisi wajitahidi kujenga vyoo bora na salama na sio lazima wajenge vyoo vya garama, sisi tunewaletea vyoo vya bei rahisi vyenye matundu ya choo yaitwayo sato hivi ni bei harisi na hufanya choo chako kiwe bora na salama,” alisema.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya mkoa wa Iringa, Dk Salim Ahmed aliwataka wananchi wa mkoa wa Iringa kuendelea kuchukua tahadhari juu ya magonjwa ya mlipuko hasa msimu huu wa mvua ambazo zimeanza kunyesha.