27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

DC KINONDONI AAGIZA MWENYEKITI WA MTAA KUHOJIWA KWA UBADHIRIFU

NA CHRISTINA GAULUHANGA-

DAR ES SALAAM

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, ameliagiza Jeshi la Polisi Wilaya ya Kinondoni, kumhoji Mwenyekiti wa Mtaa wa Kijitonyama, Philip Komanya, baada ya Sh milioni 4.5 za uzoaji takataka mtaani kwake kupotea katika mazingira ya utata.

Pia ameagiza jeshi hilo kumhoji Komanya kwa tuhuma za upotevu wa Sh 52,000 alizochangisha kwa kila mwananchi wa kata yake na kupotea bila kufanya kazi iliyokusudiwa ya ujenzi wa mtaro.

Baada ya kauli hiyo polisi walimchukua Komanya kwa ajili ya mahojiano.

Amri hiyo aliitoa jana baada ya Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama, Elizabeth Minga, kusoma ripoti ya kata hiyo na kuelezea deni la Sh milioni 4.5 wanalodaiwa na mkandarasi wa kuzoa taka ngumu.

Elizabeth alieleza kuwa wanashindwa kulipa deni hilo kwa sababu fedha walizochanga wananchi za ukusanyaji takataka zimepotea hazionekani katika akaunti wala ofisini.

Pia alisema Komanya alikuwa na akaunti mbili alizokuwa akiingiza fedha kinyemela hivyo wameamua kuifunga moja.

Maelezo hayo yalisababisha Hapi kucharuka na kuagiza polisi kumchukua Komanya na kwenda kufanyiwa mahojiano aeleze fedha alikozipeleka.

Hapi alisema hakubaliani na kitendo cha viongozi kukiuka maadili hivyo uchunguzi ufanywe na atakayebainika kuchukua fedha hizo hatua za kisheria zichukuliwe.

“Nimepata malalamiko kwa mkandarasi anadai deni, mmeshindwa kulipa naomba hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya atakayebainika kutumia fedha za umma vibaya,” alisema Hapi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles