23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

DC Ileje aahidi kusimamia kikamilifu fedha za miradi ya maendeleo

Na Denis Sekondo, Ileje

Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, Anna Gidarya amesema Serikali imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi, hivyo fedha zilizotolewa wilayani humo zitasimamiwa kuhakikisha zinatumika kuwahudumia wananchi.

Anna ameyasema hayo jana Februari 25, 2022 wakati wa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali mbali inayotekelezwa wilayani Ileje na kusisitiza kuwa maagizo ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Rais Samaia Suluhu ya kusimamia miradi yanatekelezwa ipasavyo.

“Maelekezo ya serikali ni kuhakikisha fedha zilizotolewa zinaelekezwa kwenye miradi iliyotolewa na kuhakikisha ukaguzi unafanywa mara kwa mara na waliopewa kazi ya kusimamia wanatimiza majukumu yao bila kusimamiwa.

“Lakini pia maelekezo ya Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu ya kututaka kusimamia miradi yanatekelezwa kikiamilifu ili kuwaletea wananchi maendeleo kamaa ambavyo imekuwa ikielekeza ilani ya CCM na Serikali ya awamu ya sita kwa ujumla,” amesema Gidarya.

Kwa upande wake Katibu wa CCM wilayani humo, Hassan Lyamba amempongeza mkuu huyo wa wilaya na Mkurugenzi wa Ileje kwa usimamizi mzuri wa Ilani na kuwasihi kuendelea kushirikiana ili matakwa ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo yatimie kwa muda mwafaka.

“Nikupongeze mkuu wa wilaya na Mkurugenzi kwa namna ambavyo mmekuwa mkisimamia vizuri miradi ya maendeleo lakini pia usimamizi mzuri wa ilani ya CCM kwa ujumla kwani,” amesema Lyamba.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ileje, Hebron Kibona.

Kwa pamoja wajumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Ileje wametoka ushauri kwa wataalamu kutumia taaluma zao kusimamia miradi kwa kutekeleza Ilani ya CCM huku wakisisitiza ubora wa miradi iendane na fedha zilizotolewa.

Baadhi ya miradi iliyokaguliwa na kamati hiyo ni pamoja na ujenzi wa kituo cha afya kata ya Ndola, ujenzi shule mpya kitongoji cha Ipapa kijiji cha Isongole, maeneo ya uwekezaji kijiji cha Isongole, ujenzi wa madarasa na choo shule ya msingi Ipanga kata ya Mbebe, mradi wa maji kijiji cha Ishinga kata ya Itale pamoja na ujenzi wa maabara shule ya sekondari Steven Kibona kata ya Kalembo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles