25.5 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

DC Bariadi aonya walimu watoro

Erasto Sima

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu, Erasto Sima

Na Samwel Mwanga, Simiyu

MKUU wa Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu, Erasto Sima, amewatahadharisha walimu watoro katika shule za msingi na sekondari wilayani hapa na kusisitiza wale watakaobainika kutoripoti kwenye vikao vyao watachukulia hatua za kisheria na kinidhamu.

Sima alisema hayo juzi mjini Bariadi, alipokuwa akizungumza na walimu wakuu wa shule za msingi, sekondari, waratibu wa elimu wa kata pamoja na maofisa elimu wa wilaya hiyo.

Sima aliwataka walimu wakuu na wakuu wa shule kushirikiana na waratibu elimu wa kata kuhakikisha wanasimamia suala la walimu watoro na kufanya ukaguzi wa mahudhurio ya walimu mara kwa mara.

“Naagiza maofisa elimu kata hakikisheni mnafanya ukaguzi wa kila siku ndani ya kata zenu, kuangalia mahudhurio ya walimu, mbali na hilo nitafanya ukaguzi kwa kushirikiana na ofisa elimu wilaya pamoja na mkurugenzi wa halmashauri na wakaguzi wa elimu kwa kushtukiza kuangalia mahudhurio  ya walimu,” alisema.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya, Wilaya ya Bariadi inakabiliwa na tatizo kubwa la walimu watoro na kubainisha anapata taarifa kutoka kwa walimu wakuu kuna kiwango kikubwa cha utoro na kusababisha elimu kushuka.

Mkuu huyo wa wilaya pia aliwataka watumishi wa umma, hasa wa idara ya elimu kutojihusisha na kuonya atakayebainika atamfukuza kazi.

“Wewe ukiwa mtumishi wa serikali ukitaka kufanya shughuli za kisiasa ni vizuri ukaacha kazi serikalini ukaendelea na harakati zako za kisiasa na siyo kufanya siasa, lakini bado ni mtumishi wa umma nikikugundua tu nitakufukuza kazi na hasa walimu walio wengi ndio wamejiingiza katika suala hilo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles