27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

DC Bariadi aipa siku saba Bodi ya Pamba kusambaza mbegu kwa wakulima

Derick Milton, Simiyu



Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, ametoa siku saba kwa Bodi ya Pamba nchini, kuhakikisha inasambaza mbegu za kutosha kwa wakulima kutokana na kuwepo kwa tatizo la upungufu mkubwa wa mbegu hizo katika msimu huu wa kilimo.

Hatua hiyo imetokana na hali mbaya upatikanaji mbegu za pamba hali iliyosababisha wakulima katika Wilaya ya Bariadi, kufurika kwenye maghala ya pamba kwenye vijiji vyao kwa ajili ya kupata mbegu hizo zinazotolewa na Bodi ya Pamba bure.

Kiswaga amesema kuwa Wilaya hiyo inahitaji kiasi cha tani 4,000 za mbegu za pamba, lakini mpaka sasa ni tani 1,370 pekee ndizo zimeletwa na Bodi ya Pamba wakati msimu wa kilimo hicho ukiwa tayari umefunguliwa.

Mbali na hilo, Mkuu huyo wa Wilaya huyo amesikitishwa na kitendo cha bodi hiyo kusambaza katika wilaya yake mbegu zenye manyoya peke yake badala ya mbegu zilizoondolewa manyoya Quton (UK MO8) wakati wilaya yake ni ya pili kitaifa katika uzalishaji wa zao hilo.

“Sisi ndiyo wazalishaji wakubwa wa pamba hapa nchini, tunashika nafasi ya pili, lakini leo Bodi ya Pamba wanatufanyia hujuma, wametuletea mbegu zenye manyoya tu, Quton hatujaletewa sisi, wamepelekewa kwenye mikoa mingine ambayo uzalishaji wake ni mdogo sana,” amesema Kiswaga.

Katika malalamiko yao, wakulima hao wamelalamikia bodi ya pamba kushindwa kuleta mbegu za kutosha, ambapo wengi wamepewa mbegu kidogo kuliko mahitaji halisi yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles