29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

DC AWATAKA BODABODA KUITUMIA BENKI YA NMB

Na MWANDISHI WETU

-MKALAMA

MKUU wa Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Jackson Masaka, awahamasisha madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda, kusajili vikundi vya ujasiriamali kama njia ya kujitegemea ikiwemo kupata mikopo kutoka Benki ya NMB ambayo imezindua tawi jipya wilayani humo.

Hayo aliyasema juzi alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Mkalama, ambalo limefunguliwa kwenye eneo la makao makuu ya wilaya hiyo, Ndunguti.

Alisema kufunguliwa kwa tawi hilo kumesogeza karibu zaidi huduma mbalimbali ikiwemo ya mikopo zinazotolewa na Benki ya NMB kwa wakazi wa wilaya hiyo.

“Kwa hiyo ninyi madereva wa bodaboda changamkieni fursa sasa kwani NMB imesogeza huduma. Huu ni wakati mwafaka wa kuboresha shughuli zenu, msilale changamkeni, jiungeni kwenye vikundi vilivyosajiliwa muweze kupata mikopo itakayokuza mitaji yenu,” alisema DC Masaka.

 

Mkuu huyo wa wilaya aliipongeza benki hiyo kwa kuwahamasisha baba na mama lishe, kuchangamkia fursa mbalimbali kupitia mikopo chini ya akaunti ya Fanikiwa.

“Niipongeze NMB kwa kubuni bidhaa hii ya akaunti ya Fanikiwa kupitia akaunti hii wajasiriamali hasa wadogo wataweza kupata mikopo kati ya shilingi 500,000 hadi milioni 30,” alisema

Awali akizungumza kwenye uzinduzi wa tawi hilo, Kaimu Meneja wa Kanda ya Kati wa NMB, Yasin Mfinanga, alisema hatua hiyo ni mwendelezo wa  NMB katika kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli kwa kuhakikisha wanaisaidia Serikali kuboresha maisha ya jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles