32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

DC akerwa wasichana kunyanyua matiti

BENJAMIN MASESE -Bunda

MKUU wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili amesema anachukizwa na kitendo cha mabinti wengi kunyanyua matiti juu kwa kutumia sidiria na kuyaacha wazi yakiwa na sura ya uvimbe kama sehemu ya kivutio kwa wanaume.

Lakini cha kushangaza wanapopata ujauzito na kujifungua, hushindwa kunyonyesha watoto wao.

Pia aliwataka wanaume kukataa kuoa au kuwa na uhusiano na mabinti waliokeketwa kwa kuwa wametenda dhambi ya kumkosoa mwenyezi Mungu katika uumbaji wake wa sehemu za siri, na kwamba hakuna tena utamu wala raha watakayopata wakati wa tendo la ndoa.

Kauli hiyo aliitoa wakati wa kampeni inayoendelea wilayani humo ya kuhamasisha jamii kuamsha ari ya kutokemeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto iliyolenga kutekeleza mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili (Mtakuwwa) ya 2017/18 na 2021/22 chini ya ufadhili wa Shirika la Kivulini.

“Hawa mabinti wetu jamani wanakoelekea si mahali pazuri, unakutana na dada kanyanyua matiti juu na kuyaacha wazi upande wa juu, huku akiwa ametengeneza umbo la uvimbe kama sehemu ya kivutio kwa wanaume, lakini ukimwangalia kwa uharaka utadhani hajawahi kubeba mimba, kumbe ana watoto zaidi ya wawili.

“Cha ajabu mabinti wamekuwa na tabia ya kutonyonyesha watoto wao, badala yake wanawapa wanaume kunyonya wakati wakiwa katika raha zao, hii tabia si nzuri.

“Watambue kutonyonyesha ni kumnyima mtoto haki yake, ni ukatili kwa mwanawe na kibaya zaidi hawajui kitendo wanachofanya kinawasababishia saratani ya matiti,” alisema.

Alisema pia amegundua baadhi ya jamii wilayani humo huwakeketa watoto wa kike wakiwa wachanga ili kukwepa mkono wa Serikali.

Katika hatua nyingine, alipiga marufuku Mkurugenzi wa Mji wa Bunda, Janeth Mayanja kutowahamisha walimu wanaopatikana na kesi za kuwapa mimba au kuwa na uhusiano na wanafunzi wao, badala yake awaache hapo ili washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.

“Naomba viongozi wa Serikali tuwe kitu kimoja, kuanzia mkurugenzi, polisi, maofisa elimu wa wilaya hadi kata ili kudhibiti mimba shuleni.

“Ngoja niwatolee mfano mmoja, hivi karibuni tumefanya msako katika nyumba za kulala wageni, cha ajabu unakutana na mwalimu akiwa na mwanafunzi gesti.

“Hebu jiulize mwanafunzi ametokaje kwao na kwenda gesti, na asubuhi unamuona shuleni tena anafundishwa na mwalimu yule yule, hapa kuna tatizo ambalo kuanzia wazazi hadi kwetu tuwe kitu kimoja,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles