23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Fountain Gate Academy yasaidia yatima

Mwandishi Wetu -Dar es Salaam

WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Fountain Gate Academy ya Tabata, Dar es Salaam, wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto wanaoishi vituo viwili tofauti vya kulelea yatima.

Vituo vilivyonufaika na msaada huo ni Yatima Group Trust Fund kilichopo Magomeni Mikumi na Umra Orphanage Center cha Mbagala Chamanzi ambavyo vilipata nguo, sabuni za kufulia na kuogea, sabuni za unga, mchele, unga, viatu dawa za meno na miswaki.

Msaada huo ulikabidhiwa kupitia taasisi ya Fountain Gate Academy ijulikanayo kama Fountain Gate Foundation.

Ulikabidhiwa na Meneja wa Fountain Gate Foundation, Janeth Chijanga ambaye alisema wamekabidhi msaada huo katika maadhimisho ya Siku ya Charity ambayo huifanya kila mwaka.

Janeth alisema taasisi hiyo imekuwa ikifanya tukio hilo kila mwaka kama sehemu ya kurudisha kwa jamii sambamba na kutoa somo kwa wanafunzi wake kufanya matendo ya huruma.

Alisema kila mwaka wamekuwa wakiadhimisha siku ya utoaji kwa kutoa mahitaji mbalimbali vituo vya kulelea yatima.

“Tunawajengea wanafunzi wetu moyo wa kujitolea kusaidia wenye mahitaji, ndiyo sababu ya kuanzisha Fountain Gate Foundation ili kusaidia watoto mbalimbali wenye mahitaji, tunaamini hawa watoto watakua wakiwa na moyo wa kusaidia wengine,” alisema.

Baba mlezi wa kituo cha Yatima Group Trust Fund, Haruna Mtandika, aliishukuru Fountain Gate Academy na Fountain Gate Foundation kwa matendo ya huruma wanayofanya kwa jamii ya wahitaji.

Alisema msaada huo umekuwa faraja kwao na kuiomba jamii kuiga mfano huo kwa kusaidia wengine na pia ikumbuke jukumu la kupunguza watoto wanaoishi katika mazingira magumu ni la kila mmoja.

Mlezi wa Kituo cha Umra, Rahma Kisumba, aliishukuru shule hiyo na taasisi yake kwa kuwajali watoto wanaoishi mazingira magumu na kuiomba jamii iige mfano huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles