26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

DC aguswa na misaada ya The Desk and chair Foundation

Na Sheila Katikula, Mwanza

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Amina Makilagi ameipongeza taasisi isiyo ya kiserikali ya The Desk & Chair Foundation iliyopo jijini hapa kwa kuonyesha upendo kwa  kutoa misaada mbalimbali ya kijamii ambayo imesaidia kutatua changamoto tofauti za kijamii.

Mkuu wa Wilaya wa Nyamagana,Amina Makilagi (kushoto) akipokea msaada wa madawati 348 kutoka kwa Mwenyekiti wa  Taasisi ya The Desk & Chair Foundation, Sibtain Meghjee, kulia. Picha|Sheila Katikula.

Amina ametoa pongezi hizo jana wakati akipokea msaada wa madawati 348 yaliyotolewa na taasisi hiyo kwa lengo la kupunguza uhaba wa madawati kwenye shule mbalimbali wilayani hapa na kusisitizani vyema taasisi na makampuni kuiga  mfano wa The Desk & Chair Foundation.

Alisema serikali inatambua juhudi zinazofanywa na taasisi hiyo ikiwemo kuwakatia bima za afya watu wenye mazingira magumu, kutoa taa za sola kwa wanafunzi, kufunga taa za sola kwenye nyumba 420 za nyasi  vijijini, kugawa baiskeli 600 kwa watu wenye ulemavu, kujenga madarasa.

Hata hivyo amewataka wananchi ambao walipewa fedha za mkopo  wa bila riba na taasisi hiyo kurekesha ili na wengine waweze kunufaika na mradi na kuufanya ubakie kuwa endelevu.

Naye Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sibtain Meghjee amesema madawati hayo yamefadhiliwa na familia mbili wazaliwa wa Mwanza wanaoishi Uingereza na Canada ambao ni familia ya marehemu Mzee G.B Damji.

Mwenyekiti wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya The Desk and Chair Foundation, Sibtain Meghjee akizungumza  kwenye hafla ya kukabidhi madawati 348 iloyofanyoka kwenye uwanja wa gand hall uliopo wilayani Nyamagana. Picha| Sheila Katikula.

Amesema familia hiyo imekuwa ikifadhili mambo mengi haswa kwenye elimu kwani siku za nyuma walijenga madarasa,vyoo na kutengeneza madawati Kibara mkoani Mara ambako waliishi kama Meneja wajenery  ya Kibaha.

“Familia  ya marehemu Andani ambayo ilikuwa ikiishi Malampaka ndiyo walifadhili madawati 200 kati ya haya 348 ya leo. Tunaomba madawati  50 ukabidhi kwa shule ya shule ya msingi Holy Face la jimbo kuu katoliki la Dodoma, na madawati 40 tulikabidhi siku ya mwenge  kwenye  shule ya Balale na madawati 25 tunakabidhi leo kwa madrasati Fisabillilahi iliyopo wilayani Ilemela,” alisema.

Aliongeza kuwa mwaka 2020/2021 taasisi hiyo imesaidia wanafunzi zaidi ya 10000 washule za msingi na sekondari wa elimu maalum na elimu ya juu kwa kutoa vifaa mbalimbali ikiwamo vitabu,madaftari,rim,kaluleta, sare za shule.

“Hadi hivi sasa tumeweza kufadhili zaidi ya wanafunzi 300 wa masomo ya vyuo vikuu na kozii maalum takribani kwa asilimia 40 ya wanafunzi kwani wamemaliza masomo yao na kuanza kulitumikia jamii. Taasisi hiyo imefadhili ujenzi wa madarasa 12 yaliyoharibika kwenye shule mbalimbali za msingi  yakiwamo.madarasa mawili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ambayo  yanakuwa na madawati, vyoo, jiko na bafu.

“Tumefanikiwa  kufadhili madawati zaidi ya 4000 kwenye shule za msingi na sekondari za kanda ya ziwa na visiwani lengo ni kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwenye mazingira bora,” amesema.

Hata hivyo alisema taasisi hiyo ilianzisha mradi wa kukopesha mitaji midogo  midogo  ya bila riba kwa wanafunzi wa elimu ya juu na baadhi ya watu kukataa kurejesha mara baada ya kukopa na kupelekea kufeli kwa sababu ya  wakopeshwaji kutorudisha mikopo hiyo kwani kitengo hicho kufungwa rasmi.

Naye Afisa Elimu wa Maalum jijiniwa Mwanza, Peter Ndomondo aliishukru taasisi hiyo kwa kutoa msaada huo wa viti na meza  yatapelekwa kwenye shule zenye mahitaji maalum wenye ulemavu tofauti tofauti za zilizopo jijini hapa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles