27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Dawasa yatekeleza agizo la Mbarawa bandarini

Tunu Nassor, Dar es Salaam 



Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa), imeanza kuunganisha bomba kubwa la maji litakalopeleka maji katika Bandari ya Dar es Salaam (TPA).

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Meneja wa Dawasa Mkoa wa Ilala, Judith Singinika, amesema lengo la kazi  hii ni kuongeza wingi wa maji katika bandari hiyo.

Amesema Dawasa inahakikisha kuwa mahitaji ya huduma ya maji kwenye eneo lote la bandari yanafikiwa.

“Kazi hii iliyoanza juzi, itawezesha pia meli zote za abiria na mizigo zinazotia nanga katika bandari hii kubwa kuliko zote nchini zinapata maji safi na kukidhi mahitaji.

Kazi hiyo ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, alilolitoa Julai 30, mwaka huu wakati wa ziara yake ya kutambua wateja wakubwa wa maji Dar es salaam

Profesa Mbarawa aliwataka Dawasa kupeleka maji ya kutosha katika bandari hiyo ili wapate maji yaliyothibitishwa na serikali kuwa ni safi na salama kwani maji yanayoletwa na magari hayajulikani chanzo chake na hivyo lolote likitokea baada ya kutumia maji hayo italichafua taifa.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles