26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Dada wa Gavana Balali akwamisha kesi

NA KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

ELIZABETH Balali ambaye ni dada wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, marehemu Daudi Balali, amekwamisha kesi inayomkabili kuendelea baada ya mshtakiwa  pamoja na mdhamini wake kushindwa kufika mahakamani.

Kesi hiyo ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, iliyokuja jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali, ilikwama kwa sababu hakuwepo.

Akiiwakilisha Jamhuri, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai kesi ilikuja kwa kusomwa maelezo ya awali, lakini mshtakiwa pamoja na mdhamini wake wote hawapo.

Wankyo aliomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine na endapo hatatokea mshtakiwa, upande wa Jamhuri utaomba hati ya kumkamata.

Mahakama ilikubali kuahirisha kesi hiyo hadi Julai mosi, mwaka huu.

Elizabeth aliwahi kukaa gerezani zaidi ya miezi sita, akikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi ambayo yalifutwa na kusomewa upya mashtaka ya kujipatia Sh milioni 25 kwa ulaghai.

Anadaiwa kati ya Oktoba 19 na Desemba 21, 2017 Dar es Salaam alijipatia Sh milioni 25  kutoka kwa Dk. Roderick Kisenge kwa ulaghai.

Inadaiwa alijipatia fedha hizo baada ya kujifanya anamuuzia eneo la mita za mraba 900 ambalo halijapimwa lililopo eneo la Boko Dovya, Kinondoni wakati akijua eneo hilo si lake.

Alikana mashtaka na mahakama ilikubali kumpa dhamana kwa masharti ya kuwa na mdhamini mmoja, asaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni tisa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles