29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

CUF yaibuka na hoja tatu Mahakama Kuu

Viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), wakitoka nje ya Mahakama Kuu Dar es Salaam jana baada ya kufungua kesi dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi na Mwenyekiti anayetambuliwa na msajili huyo, Profesa Ibrahim Lipumba na wenzake.
Viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), wakitoka nje ya Mahakama Kuu Dar es Salaam jana baada ya kufungua kesi dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi na Mwenyekiti anayetambuliwa na msajili huyo, Profesa Ibrahim Lipumba na wenzake.

Na Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

BODI ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF), imefungua kesi ya msingi kupitia hati ya dharura katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na msajili, Profesa Ibrahim Lipumba na wanachama wengine 11.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu, Wakili wa bodi hiyo, Hashimu Mziray, alisema wamefungua kesi hiyo kuiomba mahakama hiyo mambo makubwa matatu likiwamo la kutengua barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa iliyotengua uamuzi wa vikao halali vya chama hicho kwa kumtambua Profesa Lipumba kuwa mwenyekiti wakati alishavuliwa uanachama.

Alisema jambo jingine ni kumzuia msajili asiendelee kufuatilia suala la Profesa Lipumba kufutwa uanachama na pia azuiliwe kuingilia masuala ya CUF na kubaki na majukumu yake ya kusajili vyama kwa sababu chama hicho kinataka kufanya siasa.

“Tumesajili kesi ya msingi ambayo ina mambo matatu yakiwamo ya kumvua msajili kuingilia mambo ya CUF, jambo ambalo limetufanya tuwasilishe hati ya dharura mahakamani, tunaamini kesi yetu itachukua muda mfupi kumalizika,” alisema Mziray.

Alisema lengo la kupeleka hati ya dharura mahakamani ni kutokana na hali ya hatari iliyopo ndani ya chama hicho, kwamba hadi sasa ofisi yake ya Buguruni inakaliwa na wafuasi wa Lipumba ambao si wanachama wa chama hicho.

Mziray alisema kutokana na hali hiyo, wanachama wanataka kujua hatma ya chama chao na si kulegalega kwa utendaji ambako kunaweza kuwavunja moyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles