25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri mkuu kassim Majaliwa amsimamisha kazi Mhandisi wa maji Lindi

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa

Na Mwandishi Wetu, Lindi

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Lindi (LUWASA), Mhandisi Adam Alexander kwa matumizi mabaya ya ofisi pamoja na kushindwa kusimamia ujenzi wa kituo cha kuzalisha maji katika manispaa hiyo.

Mhandisi huyo amekabidhiwa kwa Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Lindi, Stephen Chami aliyetakiwa kufanya uchunguzi zaidi juu ya suala hilo.

Waziri Mkuu alifikia uamuzi huo jana, alipotembelea mradi wa maji wa Ng’apa na kuagiza nafasi hiyo ikaimiwe na Mkurugenzi Msaidizi wa mamlaka hiyo, Mhandisi Idrisa Sengulo.

“Mhandisi huyu anakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwamo matumizi mabaya ya fedha za ofisi pamoja na kupokea mshahara bila kulipa kodi ya mapato (PAYE), kujilipa kiwango kikubwa cha posho pamoja na kusafiri kwa muda mrefu,” alisema Majaliwa.

Alisema Serikali haiwezi kuvumilia kuona wananchi wanapata shida huku watendaji waliopewa dhamana ya kuwatumikia hawaonekani kwenye vituo vyao vya kazi.

“Kamanda wa Takukuru fanya mapitio ya kina ya mshahara wake. Yeye anasema analipwa wizarani, mimi najua analipwa na LUWASA. Angalia kazi aliyokwenda kuifanya Dar es Salaam kama inalingana na siku alizokaa.

“Huyu nimemuita mimi aje huku, hadi jana alikuwa Dar es Salaam,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles