33.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

CUF watishia kuwashtaki maofisa ZAN-ID

mnyaaNA ARODIA PETER, DODOMA

WABUNGE wa Chama cha Wananchi (CUF), wametishia kuwaburuza mahakamani maofisa wawili wa Vitambulisho vya Ukaazi (ZAN-ID) kwa tuhuma za kuwanyima vitambulisho wananchi zaidi ya 20,000.
Kutokana na hali hiyo, wamesema wananchi hao wamenyimwa haki yao ya kuandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapigakura.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana kwa niaba ya wenzake, Mbunge wa Mkanyageni, Mohamed Habib Mnyaa, aliwataja maofisa hao kuwa ni Ofisa Mdhamini wa Pemba ZAN-ID, Hamad Shamata na Ofisa Vitambulisho vya Ukaazi Wilaya ya Mkoani kisiwani Pemba, Omari Ngwali.
Alisema wana ushahidi wa kutosha kutoka kwa mwanasheria wa ZAN-ID pamoja na kaimu mkurugenzi, ambao walitoa taarifa kwao, kwamba vitambulisho vyote vya Pemba vilikwishapelekwa huko mwanzoni mwa Mei na Juni 9, mwaka huu.
Kutokana na kutokupatiwa vitambulisho hivyo, Mnyaa alisema hadi kufikia juzi watu 422 wa Wilaya ya Mkoani wameshindwa kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura na kuzuia haki yao ya kujiandikisha kupiga kura Oktoba, mwaka huu.
Mnyaa, alisema awali Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, Hemed Salum Abdullah, aliwataka wabunge pamoja na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuwahamasisha wananchi kwenda kuchukua vitambulisho vyao.
Akinukuu kauli ya mkuu huyo wa wilaya, Mnyaa alisema palikuwapo na vitambulisho zaidi ya 4,000 ambavyo havijachukuliwa na wenyewe.
Alisema kinyume chake, wananchi wanapokwenda kufuatilia vitambulisho vyao wamekuwa wakipigwa danadana na maofisa hao kwa kuwaambia kwamba bado havijafika kutoka Unguja, huku wengine wakiambiwa uzalishaji umesimama.
Mbunge huyo alisema waliwasiliana na mwanasheria katika Ofisi ya Vitambulisho Zanzibar, Hamid Haji Machana, ambaye alithibitisha kwamba vitambulisho vyote vya ZAN-ID vya Pemba vilikwishapelekwa.
“Hivyo basi sisi wabunge wa Wilaya ya Mkoani tunakusudia kuwasaidia wananchi wa Kiwani (129), Mkanyageni (83), Mkoani (86), Mtambile (88) na Chambani (36) kwenda mahakamani kushtaki.
“Kama wananchi hawa hawatapewa vitambulisho vya ukaazi, maana yake ni kwamba mchakato wa upigaji kura umeharibika na hakutakuwapo na uchaguzi huru na haki,” alisema Mnyaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles