26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

CUAMM yakabidhi jengo la milioni 200 kuhudumia wenye VVU

Derick Milton, Simiyu

Shirika lisilokuwa la kiserikali linajihusisha na masuala ya Afya Doctors with Africa (CUAMM) limekabidhi kanisa katoliki jimbo la Shinyanga jengo lenye thamani ya Sh. Milioni 209.8 kwa ajili ya kuwahudumia watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi.

Mbali na jengo hilo, shirika hilo limekabidhi mradi wa maji wenye thamani ya Sh. milioni 39.5 ambapo vyote kwa pamoja vimejengwa katika zahanati ya Old Maswa iliyopo kata ya Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

Akipokea miradi hiyo Msaidizi wa Askofu jimbo la Shinyanga Paroko Kizito Victor amesema kuwa Zahanati hiyo ambayo ni mali ya kanisa imekuwa ikitoa huduma mbalimbali kwa wananchi wakiwemo watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

Kizito amewashukuru CUAMM kwa kuwajengea jengo zuri la kisasa, ambalo amesema litaongeza ufanisi wa zahanati hiyo kutoa huduma bora na nzuri huku akihaidi kulitunza na kutumika kwa matumizi yaliyokusudiwa.

“ Kanisa linawashukuru sana CUAMM kwa msaada huu wa maji na jengo hili ambalo ni zuri la kisasa, tunategemea jengo hilo kuboresha huduma zetu, kama lenyewe lilivyo ndivyo na huduma tutaenda kutoa,” amesema Paroko Kizito.

Mratibu wa Mradi wa Taste&Treat Shinyanga na Simiyu Franscesco Bonanome kutoka shirika hilo amesema kuwa wanaamini kuwa jengo hilo litaenda kuboresha huduma za watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

“ Kupitia mradi wetu wa Taste&Treat CUAMM tumeendelea kusaidiana na serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi ikiwepo kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 hakuna maambukizi Mapya,” amesema Bonanome.

Martibu wa Ukimwi mkoa akimwakilisha Mganga mkuu wa Mkoa Hamis Kulemba amelipongeza shirika hilo kwa kutekeleza maekelezo ya serikali ya mkoa ya kuhakikisha wanawekeza katika miundombinu zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles