30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

CHUO CHAANZISHA SHAHADA YA WADUDU

 

NAIROBI, KENYA

KITUO cha elimu na utafiti kinachofadhiliwa na Benki ya Dunia kimeasisiwa katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jaramogi Oginga Odinga na kinasubiri ruhusa ya kuanzishwa kwa programu za Uzamivu na Uzamili kuhusu wadudu wanaoweza kuliwa.

Taasisi hiyo inapania kubuni njia za kuzalisha wadudu hao kwa wingi bila kuharibu mazingira, ili kukidhi utashi mara baada ya wazo hilo kufanywa kuwa biashara.

Wadudu wanaoliwa sana maeneo ya Magharibi mwa Kenya, ambao wana wingi wa madini ya protini na zinki, watafanywa kuwa biashara ili kuimarisha uwepo wa chakula cha kutosha, na kuondoa dhana mbaya katika kula wadudu.

“Kwa muda mrefu senene, kumbikumbi na panzi wamekuwa wakiliwa sana Magharibi mwa Kenya na wana madini mengi ya protini na zinc. Lakini imani potofu kuwahusu umuhimu wao, imefanya ulaji wa wadudu hawa kupungua na ndiyo maana kituo hiki ni muhimu sana,” alisema Naibu Mkuu wa Chuo hicho, Stephen Agong.

Wadudu watakaoshughulikiwa mno ni pamoja na senene, kumbikumbi na panzi.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa chakula kutoka kwa wadudu, mpango huo unatazamiwa kuanza kufanyiwa kazi katika kipindi cha miezi michache ijayo na taasisi hiyo itakuwa na uwezo wa kuwapa mafunzo wanafunzi 20 wa Uzamivu (PhD) na 60 wa Uzamili ambao asilimia 35 watatoka Kenya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles