25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

CHRIS BROWN ANAVYOTESWA NA KARRUECHE TRAN

karrueche-tran-and-chris-brown-thatgrapejuice

BADI MCHOMOLO NA MITANDAO,

NANI anasema watu maarufu hawateseki kimapenzi? Atakuwa anajidanganya kwa kuwa maumivu yake hayajali umaarufu, umasikini wala utajiri.

Nyota wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, licha ya kutoka na wasichana wengi warembo na maarufu akiwemo, Rihanna Fenty, lakini bado kila siku anaumia anaposikia mwanamitindo, Karrueche Tran, aliyekuwa na uhusiano naye kimapenzi akitoka na mwanamume mwingine.

Karrueche anatambua kwamba anapendwa zaidi na Chris na kila anapoanzisha uhusiano mpya na mwanamume mwingine huweka wazi ili kumuumiza Chris na kweli maneno makali humtoka Chris kwa walio kwenye uhusiano na mrembo huyo.

Awali baada ya kuvunjika kwa uhusiano wa Chris na Rihanna huku sheria zikimkataza Chris kumkaribia Rihanna, wapenzi hao wa zamani kila mmoja alionyesha harakati za kutaka kurudiana na mwenzake, lakini sheria za mahakama zikawa kikwazo kikubwa kwa wawili hao kurudiana ndipo Chris akadondokea katika uhusiano wa kimapenzi na mwanamitindo Karrueche huku Rihanna akiangukia kwa msanii mwenzake, Drake.

Uhusiano wa Chris na mwanamitindo huyo nao haukudumu baada ya kugundulika kwamba Chris alipokuwa na uhusiano na Rihanna, alikuwa na uhusiano mwingine wa siri na mrembo, Nia Guzmann ambaye licha ya kujifungua mtoto wa Chris aliweka siri hadi alipotimiza miezi sita ndipo alipoweka wazi kwamba mtoto ni wa Chris hali ambayo ilimkasirisha Karrueche akamwacha Chris.

Wakati hayo yakiibuka, Karrueche aliona njia pekee ya kupoza moyo wake ni kutoka na wanaume wenye majina makubwa ili amuumize Chris ambaye wakati huo alikuwa akiugulia machungu ya kumkosa Rihanna na Karrueche ambaye ameendelea kutoka na wanaume wafuatao kwa lengo la kumuumiza Chris.

Memphis Depay

Baada ya kuvunja uhusiano wa kimapenzi na Chris Brown, Karrueche aliangukia kwa nyota wa soka wa timu ya taifa ya Uholanzi na klabu ya Manchester United, Memphis Depay, ambaye anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji wenye mvuto kwa wasichana nchini Uingereza.

Licha ya mchezaji huyo kutaka iwe siri lakini Karrueche alitaka kumuumiza Chris hivyo alilazimika kuweka picha zao kwenye mitandao ya kijamii kila walipokuwa katika matukio mbalimbali ya starehe.

DJ Morten

Mwanamitindo huyo hakuacha tabia yake ya kutuma picha za uhusiano wake na mwanamume yeyote kwani baada ya kuachana na mchezaji huyo wa Manchester United, aliendelea kutuma picha akiwa na prodyuza wa muziki kutoka nchini Denmark, Dj Morten, katika matukio mbalimbali ya starehe lengo lake likiwa lile lile la kumuumiza Chris Brown.

James Harden

Karrueche baada ya kuachana na Dj Morten, alidondokea katika mapenzi ya nyota wa mchezo wa kikapu anayecheza timu ya Houston Rockets iliyopo Ligi Kuu ya Marekani (NBA), James Harden, kama kawaida aliendeleza kutuma picha katika mitandao ya kijamii akiwa na mchezaji huyo.
The Game

Licha ya kutokudumu muda mrefu na James Harden, Karrueche alidondokea katika mapenzi ya nyota wa muziki wa hip hop aliyekuwa rafiki wa karibu wa Chris Brown, licha ya awali The Game kukanusha uhusiano huo kwamba hawezi kufanya hivyo kwa kuwa ni rafiki wa Chris.

Soulja Boy

Baada ya kuachana na mwana hip hop huyo, Karrueche kwa sasa anaendelea kuligawa penzi lake kwa mwanamuziki mwingine maarufu nchini Marekani, Soulja Boy, ambapo kwa sasa inaonyesha amefanikiwa kumtesa Chris Brown kwani picha za wawili hao zilimgusa Chris kiasi kwamba akatangaza bifu kwa Soulja Boy.

Chris aliweka wazi kwamba, akikutana na Soulja Boy hakutakuwa na amani kiasi kwamba Soulja Boy naye akajibu kwamba yupo tayari kupigana na Chris Brown popote watakapokutana.

Wakati tukio hilo likiendelea kumtesa Chris Brown na kuwaweka katika hali ya sintofahamu mashabiki wao ingawa Soulja Boy ametangaza kuyamaliza bila bifu na Chris ambaye kwa sasa anadaiwa kutoka na mrembo, Cydney Christine, lakini bado anaendeleza wivu na mwanamitindo Karrueche.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles