23.7 C
Dar es Salaam
Saturday, September 23, 2023

Contact us: [email protected]

OZIL: NAMSUBIRI WENGER ASAINI NA MIMI NISAINI

Arsenal v Everton - Premier League

LONDON, ENGLAND

NYOTA wa klabu ya Arsenal, Mesut Ozil, ameweka wazi kuwa yupo tayari kuongeza mkataba wa kuitumikia klabu hiyo endapo kocha wao, Arsene Wenger, ataongeza mkataba wa kuifundisha klabu hiyo.

Ozil amedai ana furaha kubwa kuwa mchezaji wa Arsenal chini ya kocha Wenger, hivyo ataendelea kuwa mchezaji wa klabu hiyo kama kocha wake ataamua kujitia kitanzi cha kuendelea kuifundisha klabu hiyo ya jijini London.

Wenger ambaye ameitumikia klabu hiyo kwa miaka 20 sasa, anatarajia kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu, lakini kocha huyo aliweka wazi kuwa ataeleza hatima yake ndani ya klabu hiyo ifikapo Aprili mwaka huu.

Wakati huo mkataba wa Ozil ukitarajia kumalizika majira ya joto mwaka 2018, pamoja na mshambuliaji wa timu hiyo, Alexis Sanchez, lakini hadi sasa wachezaji hao hawajaongeza mkataba mpya.

“Nina furaha kubwa kuitumikia klabu hii ya Arsenal, nataka kuweka wazi kwamba nitakuwa tayari kuongeza mkataba, najua mashabiki wangu wanataka niendelee kuwa hapa.

“Wengi wanajua nipo hapa kwa ajili ya Arsene Wenger, huyu ni kocha ambaye alinisajili na imani yangu ipo kwake na ninaamini hata klabu yenyewe inataka niweke mambo wazi. Ninaamini uwepo wa Wenger utanifanya hata mimi niendelee kuwepo hapa, lakini kama akiondoka basi naweza kuondoka kwa kuwa yeye ndiye aliyenileta hapa,” alisema Ozil.

Msimu huu mchezaji huyo amekuwa na mchango mkubwa ndani ya klabu hiyo ambapo amefanikiwa kufunga mabao tisa huku akitoa pasi sita za mwisho katika michuano ya Ligi Kuu pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini anachukizwa na maneno ya watu juu ya uwezo wake.

Mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo, Thierry Henry, alionesha kuwashangaa Sanchez na Ozil ambao walikataa kuongeza mkataba mpya.

“Najua kila mmoja ana haki ya kusema wazo lake, lakini maneno ya Henry hayajanifurahisha na wala hayanisumbui chochote hata kama kuna watu wengine wanazungumzo ovyo, kwa kuwa hawajui nini kinaendelea kati yangu na klabu,” aliongeza Ozil.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,699FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles