32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

China yaomboleza wahanga wa corona nchi nzima

BEIJING, CHINA

CHINA jana ilifanya maombolezo ya nchi nzima kuwakumbuka maelfu ya watu waliopoteza maisha kutokana na virusi vya corona. 

Bendera za taifa hilo zimepepea nusu mlingoti nchi nzima pamoja na kusitisha shughuli zote za burudani. 

Siku hiyo ya maombolezo iliambatana na kuanza kwa sherehe za kila mwaka za kuwakumbuka mababu wa zamani nchini China. 

Sherehe hizo zilianza kwa nchi kukaa kimya kwa muda wa dakika tatu, ili kuomboleza waliofariki, wakiwemo wafanyakazi wa afya waliokuwa mstari wa mbele na madaktari. 

Magari, treni na meli zilipiga honi na sauti za ving’ora zilisikika hewani. 

Rais wa China Xi Jinping na viongozi wengine walitoa heshima zao za kimya mbele ya bendera ya taifa mjini Beijing. 

Zaidi ya watu 3,000 China bara walifariki dunia kutokana na COVID-19.

Wakati huo huo, Benki ya dunia imeipatia Pakistan msaada wa Dola milioni 200 za Kimarekani ili kuisadia nchi hiyo kukabiliana na janga la virusi vya corona. 

Waziri mkuu wa Pakistan, Imran Khan ametangaza kuwa hatua za kuifungia nchi zitaendelea hadi Aprili 14. Msaada huo wa fedha utatumika katika hatua za ulinzi wa kijamii sambamba na kutoa chakula kwa watu maskini na vifaa vya elimu kwa mamilioni ya watoto ambao hawako shuleni. 

Pakistan imethibitisha kesi 2,686 za COVID-19 na vifo 40. 

Visa vingi vilivyothibitishwa vimeripotiwa katika jimbo la kusini la Sindh na vinahusishwa na mahujaji ambao wamerejea kutokea Iran. 

Khan amekoselewa kwa kutochukua hatua za haraka hususan kusimamisha mikusanyiko ya Tableeghi Jamaat, ambayo ilisitishwa katikati mwa mwezi uliopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles