27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kansela Angela Merkel arejea ofisini baada ya kutoka karantini

ERLIN, UJERUMANI

KANSELA wa Ujerumani, Angela Merkel amerejea ofisini kwake juzi kwa mara ya kwanza katika kipindi cha wiki mbili ziliopita. Kansela huyo wa  chama cha kihafidhina cha “CDU” alijiweka karantini baada ya daktari aliempa  chanjo kuthibitishwa kuwa na virusi vya Corona siku mbili baadaye.

Kiongonzi huyo alijitenga nyumbani kwake mjini  Berlin baada ya kugundua mnamo Machi 22 kuwa  daktari huyo  alikuwa na virusi vya Corona

Hata hivyo kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya kansela Steffen Seibert, vipimo vilibaini kuwa Merkel hajaambukizwa virusi hivyo hatari. “Tunashukuru kuwa vipimo kadha vimeonyesha kuwa kansela bado hajaambukizwa na virusi vya Corona”, Seibert alisema huku akiongeza  kuwa, sasa ataendelea  kufanyia kazi nyumbani kwake.”

Wakati akijitenga nyumbani kwake, Merkel amekuwa akifanya mikutano ya serikali kupitia kwenye njia ya video

Kulingana na utafiti uliofanyika hivi karibuni  na shirika la utangazaji la umma nchini humo “ARD” umaarufu wa Merkel umepanda   kutoka kwa raia wa Ujerumani, katika kipindi hiki cha janga la virusi vya corona, wengi wao wakiridhishwa na hatua zilizochukuliwa.

Kwa mujiibu wa utafiti huo, asilimia 88% ya raia nchini humo wanaridhishwa na hatua za  chama chake Merkel “CDU” za kudhibiti kusambaa kwa virusi vya hivyo hatari. 

Serikali ya shirikisho ya Ujerumani imetoa mikakati kadhaa ikiwemo kuwataka watu kutokaribiana mno na kuzuia mikusanyiko ya watu wengi kama mojawapo ya kuzuia kupanda kwa mambukizi ya corona.

Kulingana na takwimu za hivi karibuni za chuo kikuu cha Johns Hopkins watu wapatao 1,107 wamefariki kutokana na virusi vya Corona na wengine 84,794 kuambukizwa nchini Ujerumani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles