Mwandishi Wetu
SERIKALI ya China imesema utamaduni baina ya nchi hiyo na Tanzania utaendelea kuwepo na wamepanga kufanya matamasha mbambali kwa siku zijazo.
Hayo yamesemwa juzi jijini Dar es Salaam na Mwambata wa Ubalozi wa nchi hiyo, Wang Sping wakati wa hafla ya kuukaribisha mwaka mpya uliopewa jina la Panya kwa kalenda ya China.
Alisema kwamba kwa muda mrefu Serikali ya China na Tanzania zimekuwa na ushirikiano mkubwa katika nyanja mbalimbali ikiwamo sekta ya utamadauni hivyo hawana budi kuudumisha.
“Kwa kuwa tumekuwa na ushirikiano wa muda mrefu ni lazima tuendelee kuudumisha, kwa kulizingatia hilo tumepnga kufanya matamasha mbalimbali ya kiutamaduni katika siku zijazo,”alisema Sping.
Kwa upande wake Balozi wa zamani wa Tanzania nchini China, Meja Jererali mstaafu, Abdulrahman Shimbo ambaye alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa aliwapongeza wananchi wa China kwa jinsi walinavyozingatia mila na utamaduni wao.