Cardi B kukimbilia siasa

0
907

New York, Marekani

NYOTA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Belcalis Almanzar maarufu kwa jina la Cardi B, ameweka wazi nia ya kutaka kuingia kwenye siasa.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 27, alitumia ukurasa wake wa Twitter na kuweka wazi nia hiyo kwa ajili ya kutaka kupigania amani kwa wananchi.

“Nadhani natakiwa kuwa mwanasiasa, naipenda serikali japokuwa mambo wanayoyafanya kwa sasa sikubaliani nayo, nimekuwa nikifuatilia video za matukio yanayoendelea ya kivita, bila ya kujali tuna uwezo wa silaha za kivita, watu wanatakiwa kuwa na amani,” alisema Card B.

Msanii huyo aliyetamba na wimbo wa ‘Bodak Yellow’ aliongeza kwa kusema anatakiwa kwenda shule kwa ajili ya kujiweka sawa mambo ya kisiasa ili aweze kuja kuwa mmoja kati ya viongozi bora.

Kutokana na ujumbe huyo baadhi ya mashabiki walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa msanii huyo anafaa kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi wa 2020.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here