26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Chifu Yemba apinga kufukuzwa uongozi CUF

Na Aziza Masoud, Dar es Salaam
MJUMBE wa zamani wa Baraza Kuu la Chama Cha Wananchi (CUF), Chifu Lutayosa Yemba amekata rufaa kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Seif Sharif Hamad kupinga uamuzi wa kufukuzwa akidai kuwa taarifa iliyotolewa na kusababisha uamuzi huo ni ya uongo.
Chifu Yemba ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Shinyanga alikuwa mpinzani wa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba katika kuwania uenyekiti wa chama hicho kwenye uchaguzi ndani ya chama hicho uliofanyika mwaka jana.
Alivuliwa uanachama na Baraza Kuu katika kikao kilichofanyika Juni 3 kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za chama pamoja na kutumia vibaya jina la mwenyekiti wa chama hicho.
Akizungumza na gazeti hili, Chief Yemba alisema chama hicho kilikuwa kimepanga kumfukuza tangu awali kutokana na msimamo wake ndani ya vikao vya chama.
Chifu Yembe alisema kwa sababu hiyo iliundwa kamati ya kuchunguza taasisi anayoiendesha na zikakusanywa taarifa za uongo kupata sababu ya kumfukuza.
“Zilikuwapo kamati tatu zilizonichunguza nasikitika walitoa taarifa za uongo kulilazimisha baraza lichukue uamuzi.
“Waliamua kuwarekodi watu kwa maelekezo yao binafsi na kwa makusudi wakatumia maneno hayo kama uthibitisho… taratibu walioutumia kunifukuza sijaridhika nimekataa rufaa kupinga uamuzi wa baraza,”alisema Chifu Yemba.
Alisema uchunguzi wa tuhuma dhidi yake ulifanyika kimya kimya katika mikoa ya Shinyanga, Singida na Dodoma ambako anaendesha taasisi hiyo na ulifanywa kwa chuki za wahusika ambao walidhamiria kuhakikisha anatoka ndani ya chama hicho.
Kwa mujibu wa Chifu Yemba baada ya uchunguzi huo hakupewa nafasi ya kujitetea wala hakuwai kusomewa mashtaka badala yake baraza lilimpa hati ya mashtaka nusu saa kabla ya kikao cha kutoa uamuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles