24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

CHAMA CHA JUBILEE CHAWAZAWADIA MAGARI WALIOUTOSA UPINZANI

NAIROBI, KENYA


WABUNGE kutoka jamii ya Wakamba ambao walihamia Chama cha Jubilee kutoka chama cha upinzani cha Wiper, wamepewa magari mapya aina ya Prado kila mmoja ili kumpigia debe Rais Uhuru Kenyatta katika eneo hilo.

Bidhaa nyingine za kampeni zikiwemo fulana na mabango ya Jubilee zinazogharimu Sh milioni 60 zilikabidhiwa kwa wabunge hao waliofanikiwa kuchukua jukumu la kampeni za rais kutoka kikundi cha wataalamu waliokuwa wakitaka kuzisimamia.

Mbunge wa Mbooni, Kisoi Munyao alisema mali hizo zilidhaminiwa na mfanyabiashara Peter Muthoka, ambaye ni mwenyekiti wa zamani wa kampuni ya magari ya CMC Motors.

“Tumepewa pia trela mbili zitakazotumika katika misafara ya kampeni eneo hili na mengine yataletwa hivi karibuni,” alisema Munyao.

Mbunge huyo pia alisema makundi, ambayo yanampigia debe Rais Kenyatta Ukambani yamesuluhisha tofauti zao.

Mizozo kati yao ilitokea kwa sababu ya ushindani kuhusu nani wa kumfikia rais kwa urahisi zaidi na pia kuhusu usimamizi wa rasilimali kubwa zitakazotumiwa katika kampeni hizo.

Wabunge hao walisema wamepata shida tangu mwaka 2014 walipoihama Wiper kwa hivyo haitakuwa haki kwao kusimamiwa na wengine kwenye kampeni.

“Hawa ni watu gani wanaojidai wanamsaidia rais wakati huu? Walikuwa wapi tulipokuwa tunatukanwa na kuitwa wasaliti wa jamii ya Wakamba?” aliuliza Mbunge wa Mwingi ya KatiJoe Mutambu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles