Celine Dion: Nina nguvu ya muziki

0
1336

celine-dionPARIS, UFARANSA

MKALI wa sauti, Celine Dion amesema kwamba ameachwa na mume wake, Rene Angelil akiwa na nguvu za kufanya muziki.

Angelil alipoteza maisha Januari 14 mwaka huu kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani, lakini Celine amedai kwamba japokuwa mume wake amefariki bado amemuacha katika mazingira mazuri ya kuendelea kufanya muziki.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, msanii huyo mwenye umri wa miaka 47, amewashukuru mashabiki duniani kwa kumsapoti katika kipindi kigumu tangu kifo cha mume wake.

“Asanteni sana mashabiki wote ambao mmekuwa pamoja na mimi katika kipindi kigumu tangu kifo cha mume wangu, ninaamini kwa sasa naweza kuanza kufanya kazi zangu za muziki kutokana na nguvu alizoniachia mume wangu,” aliandika Celine kwenye Instagram.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here