27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

CDU kumchagua mwenyekiti mpya

BONN,UJERUMANI

CHAMA cha Christian Democratic Union (CDU), kimetangaza kuanza mchakato wa kumchagua Mwenyekiti wake mpya ili kurithi mikoba ya Kansela Angela Merkel ambaye anatarajiwa kung’atuka katika uongozi wa ndani ya Chama na Taifa.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho na kuripotiwa kwenye vyombo vya habari zimesema kuwa, wajumbe wa CDU wanatarajiwa kukutana ili kumchagua kiongozi mpya ambaye huenda akasaidia kujenga mustakabali wa kisiasa kwa ajili ya kizazi kijacho.

Mshirika wa karibu wa Angela Merkel na ambaye wakati mmoja alikuwa mpinzani wake, Annegret Kramp-Karrenbeauer, ndio wanaozingatiwa kuwa mstari wa mbele kupata wadhifa wa kukiongoza chama hicho cha siasa za wastani za mrengo wa kulia.

Kansela Merkel alitangaza miezi miwili iliyopita kuwa ataachia wadhifa wake ndani ya chama, ijapokuwa anapanga kumalizia muhula wake wa sasa wa ukansela.

Kinyang’anyiro cha kupata kiongozi mpya kilichotarajiwa kufanyika jana nchini humo kilikuwa kati ya Katibu Mkuu wa CDU, Annegret Kramp-Karrenbeauer, Freidriech Merz, kiongozi wa zamani wa kundi la wabunge wa Chama cha CDU ambaye ana mtazamo wa kihafidhina zaidi na amekuwa nje ya siasa za mstari wa mbele kwa muongo mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles