26.4 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

CCM YATOA RATIBA YA VIKAO DODOMA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetoa ratiba ya vikao vyake vya kitaifa vya jumuiya za chama.

Jumuiya hizo ni Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Umoja wa Vijana (UVCCM) na Jumuiya ya Wazazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole vikao hivyo vitaketi kwa mujibu wa Katiba ya Chama na kanuni zake.

“Vikao hivi vya taifa vitahitimisha zoezi la kidemokrasi la uchaguzi wa chama chetu ulioanzia ngazi ya mashina mwanzoni mwaka huu hadi kukamilika kwa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa,” ilisomeka taarifa hiyo.

Aidha, taarifa ilitaja kuwa Desemba 14 mwaka huu, Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) itafanya kikao chake kitakachofuatiwa na Kamati Kuu itakayoketi Disemba 15, mwaka huu.

Kwamba NEC itaketi Disemba 17 na  mkutano mkuu utafanyika Disemba 18 na 19.

“Vikao vyote vitafunguliwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli.

“Kikao cha UWT kitafungwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama huku kikao cha UVCCM na Wazazi vikifungwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein,” ilisomeka.

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,  Gerson Msigwa, jana alitoa taarifa iliyoeleza kuwa Rais Dk. Magufuli aliwasili mkoani Dodoma ambako atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru zitakazofanyika Desemba 9, katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Katika hatua nyingine, jana CCM kilitoa ratiba ya uchukuaji fomu kwa wanachama waotaka kuwania uongozi katika uchaguzi mdogo wa majimbo matatu na kata sita.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Polepole kwa waandishi wa habari, wanaotaka kugombea ubunge watachukua fomu katika ofisi za wilaya za chama kuanzia Disemba 5 hadi 9, mwaka huu kwa gharama ya Sh 100,000.

“Wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo watapiga kura za maoni Disemba 12 mwaka huu na kamati za siasa zitajadili na kutoa mapendekezo kwa kamati kuu za siasa ngazi ya mkoa siku hiyo hiyo,” alisomeka taarifa ya Polepole.

Kuhusu udiwani, taatifa hiyo ilisomeka kuwa wagombea watatakiwa kuchukua fomu katika ofisi za kata, Disemba 5 hadi 8 mwaka huu kwa gharama ya Sh 10,000.

Taarifa hiyo ilisomeza zaidi kuwa uchujaji, mapendekezo na vikao vya uteuzi vitazingatia misingi ya maadili na kuhakikisha waombaji wanaakisi uaminifu, uchapakazi, heshima kwa watu, nidhamu kwa chama na wanatambulika na umma kwa nafasi zao katika jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles