30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

CCM yaonya wanaoanza kampeni mapema

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimewakumbusha watakaowania nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa kuwapata viongozi ndani ya chama mwakani kwamba muda wa kampeni bado na ukifika wataarifiwa na kufanya hivyo ni kinyume cha maadili chama na Jumuiya.

Hayo yameelezwa leo Desemba 22,2021 na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi Taifa jijini Dodoma.

Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.

Kanali Lubinga amesema mwaka 2022 ni mwaka wa uchaguzi wa ndani ya chama na jumuiya zake ambapo amedai uchaguzi maana yake ni mfumo wa kijamii ya kistaarabu kupata uongozi, kuendesha jumuiya na kwa lugha ya kisiasa ni sehemu ya kidemokrasia.

Katibu huyo wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa amesema chama kina imani uchaguzi huo utaendeshwa kwa ustaarabu na kanuni za Chama na Jumuiya lakini amedai kampeni zake bado muda na ukifika wataariwa  na wote ni lazima wazifuate.

“Iko minongono miongoni mwenu mmeanza kupiga kampeni, hii ni kinyume cha maadili ya chama chetu na Jumuiya, kibaya zaidi tunasikia watu wanabeba viongozi na wengine wameisha anza kutoa rushwa na kupokea ni vema ukaacha wala usithubutu hakuna kisichofahamika.

“Simu yangu inazo WhatsApp zenye ushahidi na Katibu Mkuu wetu wa CCM anahafamu yote, chama kimelazimika kufanya mabadiliko ya viongozi kutokana na mwenendo usioridhisha na hakitasita kuchukua hatua,” amesema Lubinga.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Dk. Edmund Mndolwa amesema jumuiya imejipanga kulipa madeni mbalimbali ambayo wamekuwa nayo pamoja na kushughulikia migogoro ya mipaka ya shule zake.

“Kutoka sasa kila fedha tutakazozipata tutatoa asilimia na kuweka fungu la kulipa madeni, haiwekekani tunasemwa huko nje hatulipi madeni tuna wastaafu wetu tuna wajane tuna mazungumzo na serikali hili lifanyike,” amesema amesema Dk. Mndolwa.

Naye, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Gilbert Kalima amesema wataendelea kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha makusudia yanayohitajika ndani ya jumuiya yanafikiwa.

Kwa upande wake, Katibu wa Organization ya (CCM) Taifa, ambaye ni Mlezi wa Jumuiya za chama hicho, Dk. Modeline Castica amewashukuru viongozi mbalimbali wa Jumuiya hiyo kwa kusimamia mambo mbalimbali ikiwemo katika chaguzi mbalimbali za ubunge na udiwani.

“Nimewaona kule Buhingwe nawapongeza sana hongereni sana, mmefanya kazi nzuri nawapenda mlioshiriki Kibondo na kule Shinyanga hongereni sana tukaenda kushiriki Konde pia hapa karibuni pia tumeshiriki Ngorongoro na kote tumefanya vizuri,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles